Joh Makini awatolea uvivu viongozi wa serikali na amjibu Young Killer Msodoki

Mr Suprize

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
869
Reaction score
961
Rapper mkongwe kutoka A Town, Joh Makini akiwa anawakilisha Weusi, amewatolea uvivu vingozi katika tasnia ya sanaa hapa nchini.
Mkali huyo wa ‘Waya’ amezungumzia juu ya kukosa sapoti kutoka serikalini akisema, “Kwakweli hawatusapoti kabisa yaani wanachukulia vitu kikoloni mno, unaweza ukawa unataka kushoot kwenye location ambazo zipo chini ya serikali lakini complicated man, utaambiwa leta barua fanya hivi nafikiri haya ni matatizo ya kuwa na wazee wengi kwenye system,” Joh alimuambia mtangazaji wa Ice FM, Gami Dee
Na alipoulizwa anamaanisha nini anaposema kuwa na wazee wengi kwenye system Joh alikazia zaidi,”kwasababu dunia inabadilika na vijana ndio wanarun dunia sasa kama mtu wanaendesha vitu katika kimiaka ya nyuma lazima tuchelewe kufika lazima vitu viende kisasa, muziki ni biashara na wasanii wanaweza kuchangia sana pato la taifa kwahiyo wapewe sapoti inavyohitajika.”
Kuhusiana na kauli ya Young Killer kuwa Joh anabebwa Joh alisema, “Sawa ya upuuzi ni kupuizia tu hivyo ukifuata ya wapuuzi nawe utakuwa mpuuzi.”
 
ni kweli kama pale basata wamejaa wacheza ngoma tuu na washamba waliosomea mashairi, kutoboa kwa wasanii wetu itakuwa ngumu mno, hata movies sisi watu wazima tunatakiwa tuwe na movies zetu ila hamna standard wote tunakuwa treated kama watoto ambao maadili yatatuondoka...bullshit indeed

kuhusu youngkiller dogo ni hanunga tuu hana lolote, joh kajibu vyema
 
nimependa alivyowachana viongoz vizee
 
njaa

sasa wasiosikia njaa wamesikia njaa

tunagawana msosi?

mziki ni chakula kitamu ingawa ukosefu wa pilipili unaweza kuleta tofauti kubwa

Vinega wengine hawa wanakuja

Ila sio wa Sugu
 
Sindio ao anaowaimbia kwenye kampeni wachaguliwe?
 
Serikali yetu bado inachukulia sanaa ni ngoma za kienyeji tuu, ndio maana hata wanaotakiwa kusimamia muziki na filamu mikoani wanaitwa maofisa utamaduni...yaani ni mizigo tu, ukiwaeleza chochote kuhusu filamu au muziki wanakushangaa tu.

Afisa utamaduni anachotakiwa ni kuhakikisha wacheza ngoma wanakuwepo kupokea viongozi basi, hapo majukumu yake yameisha....kunahitajika mabadiliko makubwa, wawepo wazee kwa ajili ya ngoma na sanaa nyingine na wawepo vijana kwa ajili sanaa ya kisasa kwenye filamu na muziki.
 
..karibu tena mtaani kwenye hili darasa cheza japo fair kidogo Mr. Afisa..wanazeekea ofisi please staafisha ,wasomi bado ni watumwa kwa wanasiasa.....( Joh Makini-Karibu tena track)
kumbe aliona mbali
 
et afisa utamaduni michezo na ngoma za asili[emoji13]
 
namtafuta producer aliyesuka beat ya 'ccm mbele kwa mbele ' nimpe dompo apooze koo..... the best beat ever!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…