Johari adaiwa kunaswa kwa Mganga

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
STAA wa filamu za Kibongo, Blandina
Chagula ( pichani) maarufu kama Johari, hivi
karibuni alidaiwa kuonekana akiingia
nyumbani kwa mganga wa kienyeji ( jina
linahifadhiwa) katika Kijiji cha Kibeta, mjini
Bukoba mkoani Kagera .
Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa
Johari akiwa katika bodaboda, aliingia kwa
mganga huyo wa kike anayefahamika sana
eneo hilo.
“Sijui nilikuwa namfananisha ? Nimemuona
msanii wenu hapa Kibeta akiingia kwa
mganga ila nimeshindwa kumpiga picha
maana kasimu kangu ni ka ’ tochi , labda kaja
kuweka mambo yake sawa , ” kilidai chanzo
hicho.
Baada ya kunyetishiwa habari hizi , mwandishi
wetu fasta alibonyeza namba za Johari
katika simu yake ambaye alikiri kuwepo
Bukoba kwa siku mbili kwa shughuli zake .
“Jamani siyo kila kitu muandike, mmejuaje
mimi nilienda Bukoba , naomba hii isiwe
habari tafadhali si ulimwengu mzima ujue
mimi nimefanya nini, ” alisema Johari, mmoja
wa waigizaji nyota na mkurugenzi mwenza
wa RJ Company.
Katika kujitetea zaidi , Johari alisema
alikwenda Bukoba kwa mama yake mkubwa,
( jina linahifadhiwa) ambaye hakujua kama
anajishughulisha na mambo ya uganga kwani
hakuwahi kusikia .
“Sikupenda hii habari kabisa , lakini kiukweli
nilienda kumuona mama yangu mkubwa
nikiwa na ndugu zangu wengine, kwani
alikuwa akiumwa, sikukaa sana, nilikaa siku
mbili tu na kugeuza kwani nilikuwa nikitokea
Shinyanga kwenye msiba kama ulisikia
nilifiwa ,” alisema na kuongeza kuwa hajawahi
kupanda pikipiki kwani magari yapo tena kwa
bei rahisi .
 
Wasukuma hawan uchawi wa mapenzi wala wahaya
chezea chuchu hansyy
 
Njoo nikupeleke Kwa babu Bumbwini, Ray atarejea mwenyewe.. Kama ndie anaekupa zao macho...
 
Mastaa mna kazi kiukweli.
Kwenda kwa mganga nayo ni issue kihivyo???!!!
 
Mmh!! Mtoa habar nae anapenda umbea, vitendea kazi hana kama Dinazarde, mmh eti hakuweza kumpiga picha kwa kuwa ana simu ya torch, mbea huyu nfyuu, na nyie akina shigongo siku iz kuna smart gulio ebu wanunulieni watoa habar wenu wa vijijin, hauon sasa habar haijakamilika picha hamna, huenda huyo mtu hajamuona johar kamuota tu maana mashabiki nao hawaaminiki
 
Last edited by a moderator:
usupastaa ni mzigo wa mwiba, usupastaa kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…