Johari na Ray waja kivingine

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506



Wasanii wa filamu wanaounda kampuni ya RJ Company, Brandina Chagula ‘Johari’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wanajiapanga kuingia kwenye biashara ya kuandaa tamthilia ambazo zitakuwa zinaonyeshwa katika runinga.

RJ Company ni miongoni mwa kampuni kongwe za filamu nchini ambazo mpaka sasa imeshaandaa filamu nyingi pamoja na kuibua vipaji vipya vya waigizaji.

Akizungumza katika kipindi cha Uhondo cha EFM, mmoja kati ya wakurugenzi hao, Johari Chagula, amezungumzia mipango mbalimbali ya kampuni hiyo.

“Kwa sasa bado tunaendelea kutoa filamu kama kawaida ila tunampango mkubwa zaidi, kuna tamthilia ya runinga ambayo inakuja, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema Johari.
 
Hadi Leo bado ni. Vijana Tu?
 
Naomba physical address ya RJ COMPANY na ikiwezekana na namba zao za simu /za kampuni
 
Isije ikawa zile tamthiliya zao zinaishia sehemu ya 9 au 21 yaani ndio mwisho wa tamthiliya
Jamani Tuesday kihangala yuko wapi alitikisa na Jumba la dhahabu kipindi kile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…