Mkuu W. J. Malecela, swali lako ni zuri sana.
Suala la imani ni gumu kulizungumzia bila kuingilia uhuru na haki za waumini. Hivyo ni vizuri kuwa makini kuzungumzia masuala ya dini.
Pamoja na kuwa Osama Bin Laden amehusisha vitendo vyake (terrorism) kwa kiasi fulani na dini yake, kwa upande mwingine amehusisha na chuki zake binafsi kwa Marekani (ambazo hazihusiani kabisa na dini yake). Kama wewe ni mfuatiliaji, utagundua kuwa vitendo vyake vimeichafua dini yake na asili yake (uarabu) kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa kuwa wengi wentu tumesikia na kufahamu kuwa kikundi chake (Al-Queda) kiliundwa na kusimamia misingi gani, inakuwa si busara wala haki kuhusisha vitendo vya Osama na dini yoyote.