Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
JOHN GEORGE TERRY TOKA GHETTO LA BARKING LONDON MPAKA MITAA YA DARAJANI:
Ukitaja Viongozi bora wa timu uwanjani (Captain) na wenye mafanikio kwenye nyasi za kijani huwezi kumuacha John Terry.
Uwezo mkubwa wa kuongoza safu ya ulinzi kwa nidhamu na ubora ilimfanya Terry kuwa Baba bora katika familia yenye maadili takatifu aliwapa mashabiki wa darajan kilicho bora kwa wakati bora kutoka kwa mtu bora na kazi safi.
Uwezo wakusoma Mchezo (Ability to read the game), ukarimu wa mpira (tenacious), nguvu ya upambanaji; yes alikuwa kiongozi sahihi, akiri sahihi, na mwalimu sahihi mwenye mafunzo sahihi, kwa ujenzi wa ngome ngumu iliyokua chini yake kama chief Mangungo na msovelo yake.
Nidhamu yake uwanjani ulithibitisha kwa nini yeye ni bora na ilimlipa kwa mda mrefu sana na kumpa vikombe vyake murua kabisa na alikaa kwa mda mrefu, licha ya kuunda pacha na watu wagumu na bora pia mtu kama Marcel Desailly kutoka viunga vya Accra Ghana mpaka Jiji la Maraha (France), William Gallas na wengine wengi.
Kilicho bora hakikosi kasoro vipi kuhusu utukutu jamaa hiki kitu kwake aliona kawaida, "2002 pale West London aliingia kumbi ya starehe (disco) na Jody Morris na hata kupigana na baunsa.
Hii ilimpelekea kula tofali la mda kutoka kwa team ya taifa la Malkia, Ikumbukwe 2001 alishakula faini kwa ajili ya pombe iliyomfanya kumpa tabu mtalii mmoja toka kwa wahuni America lakini ilibidi akubali kwa muhuni wa Barking.
Ubora wake uwanjani ndio ilikua jeuri yake hii ilimfanya kuingia kikosini mara kwa mara na kuaminiwa na wakufunzi, 2003-2004 Terry anakua kaimu captain baada ya Desailly kua na majukumu ya Taifa hili lilifanyika chini ya master Claudio Ranieri.
Ikampa wasaa wakuzid Kuonyesha ukomavu wake dimbani na baada ya kustafu Desailly mpaka ujio wa Mzaramo Jose Mourinho haukua na nongwa ukambariki Terry kua captain mkuu nae hakuona hajizi akambariki the special one kombe la Ligi nae kujizawadia uchezaji bora ligi (2004-2005), bila kusahau beki bora ya UEFA Champion League.
Atake nini tena kijana wa mzee George! mateso yanamkuta Terry.
Si kwingine ni ule usiku mjini Moscow katika dimba la "Luzhniki Stadium" Terry anamzawadia Sir Alex Ferguson kombe baada ya mkwaju wa penalty yake kula bomba, huzuni inatanda na machozi yanatoka kwa mashabiki wa darajani Terry amtazame boss wake anahisi kamdhulumu atazame mashabiki aone giza.
What a magnificent performance, anapiga mzigo mkubwa usiku huo na unampa tuzo ya beki bora wa mwaka Champions League.
Hii si ya kusahau Terry anaingia kwenye record nyingine 2011 anatukumbusha ubora wake ulivyokua anakua mchezaji wa tatu aliepiga pasi nyingi Ulaya akiwa na asilimia zake 91.6% nyuma ya Xavi 93.0% na Leon Britton 93.3% Ingini ya Swansea City hii.
Usiku mwingine unalejea Ndani ya Allianz Arena kwa Babu mwenye pamba kichwani [emoji1787][emoji1787] Si mwingine ni Jupp Heynckes.
Mara ghafla huzuni inakuja kwa De Matteo baada yakukumbuka Terry ana adhabu ya red card anaingia uwanjani kwa huzuni Thomas anatupia header ya kikatili sana dakika ya 87 Matteo anatazama benchini hamuoni Terry anakumbuka yupo juu kala suti kumbe jamaa alikua kashajianda na kuvaa taji lenye dhahabu.
Muhuni mwenye uhuni wake nje ya dimba na kiongozi mtiifu ndani ya sheria 17.
Samatta msikilize Mtaalam, ila tabia mwachie yeye maana akiri zake wanazijua vijana wa London tu.
Sent using Jamii Forums mobile app