Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bara John Wegesa Heche John Heche amesema chama hicho kimejiandaa kushiriki uchaguzi mwaka huu hivyo kikisema 'no reform no election' isitafsiriwe kama hawakujiandaa.
Heche akizungumza Februari 21, jijini Arusha amesema pale ambapo Katibu Wa Halmashauri Kuu Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Amos Makalla akisema CHADEMA haijajiandaa na uchaguzi aulizwe kwa nini wagombea wa CHADEMA wakichukua fomu wanaenguliwa.
Hata hivyo Heche amesema kubwa wanalohitaji kama chama chao ni uwepo wa uchaguzi wa uhuru na wa haki ndipo watakuwa tayari kushiriki.
Ndugu Heche aambiwe kuwa habari za ccm kukataa uchaguzi huru na wa haki siyo mpya mjini. Heche na Lisu wajikite kutuelekeza wananchi ni kwa namna gani uchaguzi tutauzuia.