SI KWELI PreGE2025 John Heche hataki No reforms No election na ametangaza kugombea Tarime vijijini

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Wakuu JamiiCheck, nmekutana na Taarifa inayoeleza kuwa Jihn Heche hataki ajenda ya No reform na ametangaza kugombea ubunge jimbo la Tarime vijijini?
 
Tunachokijua
John Heche ni makamu Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Taifa, amewahi pia kuwa mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini. Chadema wana kampeni No reforms No election ikiwa na lengo la kudai mbadiliko mbalimbali ikiwemo ya sheria za uchaguzi ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025.

Madai

Zipo Taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikieleza kuwa John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa amekataa kuhusu kampeni ya “No reforms No election” na ametangaza kugombea ubunge Jimbo la Tarime Vijijini. Tazama Hapa

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia madai hayona kubaini kuwa hayana ukweli. Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao tumebaini kuwa hakuna mahali ambapo makamu mwenyekiti huyo amekataa ama kupinga kampeni ya No reforms No election ambayo ndiyo kampeni ajenda yao hivi sasa wanayokwenda nayo.

Aidha kuhusu kugombea ubunge vijijini hadi kufikia leo tarehe 22/03/2025, Heche hajatangaza eidha kupitia mitandao yake ya kijamii ama kupitia mahali popote kueleza kuwa atagombea ubunge jimbo la Tarime vijijini ama kususia no reforms no reforms. JamiiCheck imefuatilia katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Heche na kubaini hajaandika kuhusu jambo ama madai ya yeye kutaka kugombea na kukataa no reforms no election.

Heche atakuwepo pia katika uzinduzi wa kampeni ya No refoems No election utakaofanyika Kanda ya Nyasa tarehe 23/03/2025 kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Chama chao. Hivyo kutokana na ushiriki wake huo inadhihirisha madai ya kuwa amegomea no refoorms no election si ya kweli.​
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…