John Heche Kama Kuna Watu wanakufuatilia toa Taarifa Polisi

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,592
Reaction score
15,404
Nimefuatilia Clip ya John Heche kuhusiana na Kufuatiliwa na gari aina ya Toyota LandCruiser Hardtop Nyeupe, Pale unapoona Viashiria kama hivyo toa taarifa polisi ili waweze kuchunguza nchi ina watu wengi hii nadhani mnakumbuka kifo cha Chacha Wangwe baada ya kuwa na Mgogoro mkubwa na CHADEMA alipata ajali ambayo haieleweki ndugu Heche toa taarifa rasmi Jeshi la Polisi wao watakusaidia kuwachunguza wanaokufuatilia kila unapokwenda.
 
Police ipi? Police wapi? Police ya nani?
 
Me nadhani ifike hatua sasa kuanzisha uzi jf pawe na malipo

Kwani mkuu una umri gani?
Unaishi nchi gani?
 
Polisi ndio wanaomfuatilia.

Lissu alitoa taarifa mapema sana na akawapa hadi namba ya gari.
 
Lissu akiwa Dodoma alitoa taaharifa mara ngapi police Je hakushambuliwa? Sembuse hawa Askari wa October 29 waliokua wanawinda watu kama wanyama porini mpaka traffic anaonekana sare ameshika bunduki anawinda watu ndo haende kutoa taaharifa kweli? Police waliopiga watu risasi kwenye banda la video mwanza October 29 Police wa nchi hii wameoza
 
Sitoi taarifa polisi hadi upelelezi wa kifo cha Ally Kibao utakapokamilika na ule wa Tundu Lissu kupigwa risasi Dodoma maeneo yenye ulinzi wa kidigitali.
Heche,John.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…