John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anatema cheche muda huu mjini Tarime

John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anatema cheche muda huu mjini Tarime

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, John Heche leo Jumatano Februari 12, 2025, anazungumza na wananchi wa Tarime

Fuatilia hapa kinachoendelea kutoka mjini Tarime

John Heche anasema "Hapa ndio Tarime, leo nimesimama kuwashukuru wananchi wa Tarime, nyie mlioniona mwaka 2008 nikiwa mdogo sana, mkaniamini, mkaanzisha safari yangu, wakati ule watu walisema sina hata kitanda, mkasema tunataka tumchague aende akanunue Kitanda. Mnakumbuka vita mtuliyopitia mpaka mama yangu akarushiwa vitu nje ya nyumba, nyie mkasiamama na mimi, mkaniunga mkono, safari yetu ikaanza na nataka niwaambie leo mbele za Mwenyenzi Mungu tukiwa wazima safari hii itaendelea na itakwenda juu zaidi ili tuweze shirikiana kuibadilisha nchi hii"

"Lissu ametoa maelekezo na huo ndio utakuwa msimamo wetu, ambao mimi na Lissu tupo tayari kufa kwaajili ya kulinda msimamo wa Chama na tutawaongoza Wananchi, tunatambua ni watu tulio zaliwa na ipo siku moja tutaondoka duniani, tunataka tuondoke katika hali ambayo tutaacha nchi yetu ikiwa salama na madini yake na Rasilimali zake zinatumika kwa ajili ya watu wengine woto na sio kikundi cha watu wachache wanaojinufaisha, huku wengine mkiendelea kufa masikini na hamuwezi hata kula chakula"

"Tuna matatizo makubwa kwenye nchi hii, watu wetu hawana chakula wanalala njaa kwenye nchi tajiri, matibabu hakuna (tumemuona mama moja hapa anazungumza kwamba asaidiwe kutibu mtoto wake) sisi tunataka tujenge nchi ambayo wewe mwananchi utakuwa na uwezo wa kujisimamia utibiwe kama John Heche anavyoweza kwenda kutibiwa mahali popote kwasababu utakuwa na uchumi."

"Tunataka tujenge nchi ambayo wewe utalala kwenye nyumba nzuri kama ambayo analala mtoto wa Wasira kwasababu nchi hii ina uwezo huo. Tunataka kujenga nchi ambayo utatibiwa kwenye hospitali ambayo anatibiwa mtoto wa Samia Suluhu Hassan, hatutaki nchi yenye matabaka, tunataka nchi ambayo rasilimali zetu zinatumika kwaajili yetu sote"

"Matabaka haya yapo kwasababu nguvu za Wananchi zimepokwa kutoka mikononi mwao kwa kutumia vyombo vya dola, kwa kutumia Polisi, Usalama wa Taifa, kwa kutumia majeshi yetu, hizo nguvu zimewekwa kwenye mikono ya mtu mmoja anayeitwa Rais"

"Leo mjinga yeyote akiwa Rais watu wanaanza kumtukuza kwasababu ya Urais, hawawezi kuheshimu tena Wananchi wanamtukuza Rais, Wabunge wakisimama Bungeni wanatukuza Rais, Rais wa Tanzania amegeuka kuwa Mungu kwasababu yeye ndiye anayeteua Wabunge, Wenyeviti wa Vitongoji, Madiwani kwa kutumia vyombo vya dola."
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, John Heche leo Jumatano Februari 12, 2025, anazungumza na wananchi wa Tarime

Fuatilia hapa kinachoendelea kutoka mjini Tarime

John Heche anasema "Hapa ndio Tarime, leo nimesimama kuwashukuru wananchi wa Tarime, nyie mlioniona mwaka 2008 nikiwa mdogo sana, mkaniamini, mkaanzisha safari yangu, wakati ule watu walisema sina hata kitanda, mkasema tunataka tumchague aende akanunue Kitanda. Mnakumbuka vita mtuliyopitia mpaka mama yangu akarushiwa vitu nje ya nyumba, nyie mkasiamama na mimi, mkaniunga mkono, safari yetu ikaanza na nataka niwaambie leo mbele za Mwenyenzi Mungu tukiwa wazima safari hii itaendelea na itakwenda juu zaidi ili tuweze shirikiana kuibadilisha nchi hii"

Chadema ndiyo inajifia hivyo.
 
Back
Top Bottom