POTOSHI Je, ni kweli Heche amesema watatumia uhuru wa chama chao kuteka na kuumiza watu?

POTOSHI Je, ni kweli Heche amesema watatumia uhuru wa chama chao kuteka na kuumiza watu?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1


Screenshot 2026-06-10 111057.png
 
Tunachokijua
Katika kilelele cha maadhimisho ya miaka 33 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Januari 22, 2026 akiwa mkoani Mara, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara John Heche, alisisitiza kuwa uongozi wa sasa hautafanya usaliti wala kulegeza misimamo yake na kwamba kitaendelea kusema ukweli bila kuupamba, bila kujali ukali wa mazingira ya kisiasa nchini.

Madai

Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kikimuonesha Heche akisema "Tunataka kutumia nafasi hii kuwaambia serikali, kwa muda ambao sisi tunaongoza chama hiki tutatumia nafasi ya dola kuteka watu, kuumiza watu, ku-silence watu, kuumiza hata viongozi wa dini wanaokuwa na mawazo tofauti"

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?


Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia marejeo ya video umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kukata na kuunganisha vipande isivyostahili hivyo kutengeneza ujumbe ambao haukutolewa na Heche.

Kupitia video iliyochapishwa YouTube na Chadema Media TV
Heche alisisitiza kuwa chini ya uongozi wao, chama kitasimamia ukweli na kupigania ushindi wa dola bila usaliti wala kupigia magoti udhalimu, huku akibainisha kuwa nchi hii si mali ya Rais Samia wala kikundi cha watu wachache wanaotumia madaraka kuteka na kuumiza wanaotofautiana nao, bali ni mali ya wananchi wote.

"Kwa muda ambao sisi tunaoongoza chama hiki, tutakipeleka kwenye nafasi ya kwenda kushinda dola na kutimiza yale ambayo wazee wetu walitamani kuona yanatokea.

Hatutafanya usaliti, hatutamwonea mtu, hatutamwonea mtu aibu. Kama ni nyeupe tutakwambia ni nyeupe, kama ni nyeusi hatut some itamba itamba kwamba ina rangi kama bluu bluu hivi au... tutasema hii ni nini? Nyeusi. Na hatutapigia magoti udhalimu.

Na tunataka kutumia nafasi hii pia kuambia serikali; nchi hii sio mali ya Rais Samia, wala sio mali ya kikundi cha watu wachache wanaotumia nafasi ya dola kuteka watu, kuumiza watu, ku-silence watu, kuumiza hata viongozi wa dini wanaokuwa na mawazo tofauti nao... Sio mali yao!

This country belongs to us all. Ni nchi yetu sote!"
​
kumekuwa na machapisho kadhaa yanayosambazwa kupitia mitandao ya kijamii yakimhusisha kiongozi na makumu mwenyekiti wa chadema taifa john heche na nukuu inayodai kuwa alisema, "tutatumia uhuru wa chama chetu kuteka na kuumiza."

chapisho hilo linaambatana na ujumbe unaosema:"hizi si siasa za ustaarabu wala demokrasia ya kweli, bali ni kauli zinazoweza kuligawa taifa na kuingiza vijana kwenye njia hatari ya uhalifu na machafuko. kiongozi anayetamani madaraka kwa gharama ya amani ya wananchi hafai kupewa nafasi ya kuaminiwa na jamii."

Je ?ni upi halisia wa chapisho hilo ambalo linasambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
JOHN HECHE.jpg

 
Back
Top Bottom