Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ametoa wito kwa Wawakilishi wa Asasi za Kiraia (AZAKI) pamoja na Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kuzingatia suala la kupanda kwa gharama za maisha. Mnyika amesema hali hiyo ni sehemu ya athari mbaya za kiuchumi zinazowakabili wananchi wengi, ambao wanalia kuhusu ugumu wa maisha.
Mnyika pia amewataka THRDC, kwa kushirikiana na AZAKI, kuangazia suala la deni la taifa, ambalo amedai linakua kwa kasi. Akisema kuwa ni muhimu kwa taifa kuepuka kutumbukia katika mgogoro mkubwa wa madeni.
Katika ziara hiyo, THRDC kwa kushirikiana na AZAKI 300, wamewasilisha na kukabidhi vitabu vya ilani ya uchaguzi wa Asasi za Kiraia kwa mwaka 2024/2029. Lengo la kutoa ilani hiyo ni kuhakikisha mambo muhimu kwa maisha ya Watanzania yanapewa kipaumbele kuelekea chaguzi mbili zijazo, yaani uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Soma Pia: CHADEMA yakabidhiwa Ilani ya Uchaguzi kutoka kwa AZAKI 300 nchini