John Mrema hatujamfukuza CHADEMA. Puuzeni taarifa Potofu

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Siku ya kufukuzwa ikifika mtataarifiwa

Habari potofu imeandikwa kwamba Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imetangaza rasmi kumfuta uanachama Bw. John Mrema. Kwamba hatua hii imefikiwa baada ya kubaini kwamba Bw. John Mrema na kundi lake linalojiita G55 hawana nia njema na mustakabali wa Chama na wana malengo ya kudhoofisha maazimio kadhaa yaliyopitishwa.

Eti uamuzi huu umefanyika baada ya Kamati Kuu ya Chama kukutana kwa dharura na kujadili mambo kadhaa ikiwemo operesheni inayoendelea ya No Reforms, No Elelction.

Imetolewa leo Jumatatu, 07 Aprili 202

Brenda Rupia Mkurugenzi wa Mawasiliano.

Huo ni uongo
 
Ajabu ya mpanda mti kutaka mti ufe anakata matawi badala ya kung'oa mizizi,,
 

Nawashauri Watu wa CHADEMA kwamba ili kuzuia Watu wengine wenye nia ovu dhidi ya Chama chenu katika kuwadhibiti wasiweze kueneza taarifa gushi za uwongo (fake news) dhidi yenu hususani kuhusiana na Matangazo yenu ya Taarifa kwa Umma (Press Release), mnapaswa muwe mnayapatia Nambari za Kumbukumbu (Reference Numbers) hayo Matangazo yenu. Kila Tangazo lenu la Taarifa kwa Umma linapaswa liwe na Nambari yake ya pekee ya Kumbukumbu kuhusu Tangazo husika. Hii inaweza kusaidia kudhibiti masuala ya kughushi kuhusu Matangazo yenu. Katibu Mkuu wa Chama chenu Bw. John Mnyika anapaswa aanzishe Majalada Maalumu (Document Files) kuhusiana na Matangazo hayo.Mfikishieni taarifa hii ili aanzishe mikakati ya kudhibiti kughushiwa kwa Taarifa potofu dhidi yenu.
Erythrocyte
 
Chadema ! Mlikosea step! Kufanya uchaguzi wa chama ndani ya mwaka wa uchaguzi mkuu!

Kwa kifupi chama kimepoteza uelekeo 100%
 
Mama anawapelekea moto,mpk mnachanganyikiwa

Hio oktoba ndio mtapoteana kabisa
Mama anaupiga Mwingi
 
Reactions: UCD
Mama anawapelekea moto,mpk mnachanganyikiwa

Hio oktoba ndio mtapoteana kabisa
Mama anaupiga Mwingi
Mimi ni CCM ,ila Chadema ikifa, tumeliwa!
Yule bibi ataifanya visiwani kuwa Dubai,hakuna wa kumsema Wala kumwambia ubaya wa matendo yake
 
Mimi ni CCM ,ila Chadema ikifa, tumeliwa!
Yule bibi ataifanya visiwani kuwa Dubai,hakuna wa kumsema Wala kumwambia ubaya wa matendo yake
Hakuna ubaya,tutaenda kutalii badala ya kwenda mbali Dubai

Pesa itabaki jamuhuri
 
Yani mtu anayewajibika kwnye tawi afukuzwe na kamati kuu? Ana umuhimu gani wa namna hiyo?
 
Mimi ni CCM ,ila Chadema ikifa, tumeliwa!
Yule bibi ataifanya visiwani kuwa Dubai,hakuna wa kumsema Wala kumwambia ubaya wa matendo yake
Kwani umewasikia chadema wanasema chochote cha maana kuhusu huyo bibi? Hawana hoja yoyote ya msingi ya kumsema zaidi ya kupayuka porojo tu.
 
Ahahahahaha! Huyu si John Mrema si ana hela za Abdul? Tena hela nyingi tu kama alichosema Godbless Lema kwenye twitt yake? AFUKUZWE! Chadema ya Lissu isioneshe udhaifu mapema hivyo wa kutowashughulikia wasaliti! MFUKUZENI!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…