John Shibuda aungana na wabunge wengine kushutumu Mawaziri kubariki ufisadi

John Shibuda aungana na wabunge wengine kushutumu Mawaziri kubariki ufisadi

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Date: 6/16/2009

Mbunge John Shibuda (CCM) naye ameungana na wabunge wengine kushutumu Baraza la Mawaziri kubariki ufisadi nchini.

* Ahoji uzalendo wao, asema nchi inapoteza dira,mwelekeo

Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe, Dodoma

Mwananchi

HALI inazidi kuwa mbaya kwa Baraza la Mawaziri baada ya mbunge wa Maswa kwa tiketi ya CCM, John Shibuda kuliangukia tena akihoji uzalendo wake na kueleza kuwa mikataba yote mikubwa ya kifisadi imepitishwa kwa baraka za chombo hicho.

Kauli ya Shibuda, ambaye ameweka bayana nia yake ya kugombea urais mwakani, imetolewa siku moja baada ya mbunge wa Nzega, Lucas Selelii kulishushia tuhuma nzito kuwa limejaa watu wabinafsi, wasiowatakia mema wabunge wenzao na kumwomba Mungu awalaani.

Kama kawaida yake akitumia lafudhi ya Pwani, Shibuda alihoji ni kipimo gani kinaweza kutumika kupata tafsiri ya uzalendo kwa mawaziri wakati mambo hayaendi vizuri nchini?

Shibuda, ambaye alikuwa akizungumza kwa mfano na vielelezo huku akinukuu katiba, alisema mambo mengi ambayo yanaonekana kuvurugika nchini, ikiwemo mikataba mikubwa, mibovu na ya kifisadi imepitishwa na baraza la mawaziri.

“Iko wapi tafsiri ya uzalendo kwa mawaziri wetu, mambo mengi tunayaona makubwa, ikiwemo mikataba mibovu kwa nchi inapitishwa na baraza la mawaziri?” alihoji.

Mbunge huyo machachari, alifafanua kwamba, mikataba mikubwa mibovu kama ya madini yote ilipata baraka za baraza la mawaziri.


Alisema watu hawana budi kurejea katika Azimio la Arusha na TANU ambayo iliweka dira ya maendeleo ya wananchi na kujitegemea.

“Ukisoma katiba yetu inasema ni nchi ya ujamaa na kujitegemea, lakini hadi sasa hakuna misingi yoyote ya kujitegemea. Wananchi wa kawaida wanazidi kuwa maskini,” aliongeza.

Kuhusu bajeti na wakulima, alisema serikali imeshindwa kutumia mitaji iliyopo kwa kushindwa kuwekeza kwa wakulima wa pamba na sekta ya mifugo.

Alisema wafugaji na wakulima wangewekewa misingi mizuri, nchi ingeweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo na kuachana na utegemezi wa misaada ya nje ambayo ni ya mabepari ambao huleta unyonyaji.

Mbunge huyo machachari alisema ndiyo maana hadi sasa uchumi mkubwa umeshikwa na wageni na kuhoji: “Tulipigania uhuru ili iweje?”

Shibuda pia alizungumzia mradi wa vitambulisho vya taifa, akisema umefika wakati sasa mradi ukahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kuwa hakuna maendeleo yoyote zaidi ya malumbano.


Alisema vitambulisho vya taifa ni muhimu kwani ungewezesha nchi kuwa na mfumo ambao ungetambua walipakodi kutoka sekta rasmi na isiyo rasmi.

Naye mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe, alihoji watuhumiwa wa ufisadi wa kampuni ya Richmond Development (LLC) kuendelea kuwepo hadi sasa bila kuchukuliwa hatua huku wakizidi kutengewa fungu la bajeti.

Alisema mafisadi wanakwamisha maendeleo ya uchumi wa nchi, pamoja na kusababisha umaskini kwa Watanzania.

 
Nashukuru kwa Post yako naona yangu imekuja baada ya kwako so moderators najua wafanya kazi yao kuondoa bandiko langu.
Sasa ningependa kujua Role ya Raisi, Waziri Mkuu, na Wataalamu wa Sheria pamoja na jambo linalojadilia katika maamuzi ya baraza la mawaziri. Does it mean na Raisi wetu hua anabariki huo ufisadi pamoja na waziri mkuu? Kama ni Hivyo nini usalama wa Taifa Letu, na kama si hivyo Je wenzetu hao wanachukua hatua gani kulinusuru taifa na maafa haya?
 
Mkuu kishasema kuzungumzia Azimio la Arusha siku hizi watakuona wewe chizi. Shibuda ni chizi.
 
Nashukuru kwa Post yako naona yangu imekuja baada ya kwako so moderators najua wafanya kazi yao kuondoa bandiko langu.
Sasa ningependa kujua Role ya Raisi, Waziri Mkuu, na Wataalamu wa Sheria pamoja na jambo linalojadilia katika maamuzi ya baraza la mawaziri. Does it mean na Raisi wetu hua anabariki huo ufisadi pamoja na waziri mkuu? Kama ni Hivyo nini usalama wa Taifa Letu, na kama si hivyo Je wenzetu hao wanachukua hatua gani kulinusuru taifa na maafa haya?

Waziri mkuu ana kuwepo kwenye cabinet meetings. Raisi mwenyewe ndiyo bosi wa baraza la mawaziri. Kwa hiyo hamna kinacho weza kutendeka hawa waseme hawajui kitu. Wakisema hawajui kitu basi ina maana hawafanyi kazi yao ipaswavyo.
 
D@@@@mn right chizi.
I was being sarcastic by calling Shibuda a chizi. I think those who are putting down ujamaa are the chizi. Look at how they are selling our country left and right.
 
Date::6/16/2009


Mbunge John Shibuda (CCM) naye ameungana na wabunge wengine kushutumu Baraza la Mawaziri kubariki ufisadi nchini.

* Ahoji uzalendo wao, asema nchi inapoteza dira,mwelekeo

Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe, Dodoma

Mwananchi




Mbunge huyo machachari alisema ndiyo maana hadi sasa uchumi mkubwa umeshikwa na wageni na kuhoji: “Tulipigania uhuru ili iweje?”

.

Bravo Shibuda kumkoma nyani, hasa hapo umenigusa haswa!,

Yaani kweli tulipaigania uhuru ili mafisadi papa wenye uraia wa utata waje kutanua sie tubaki kutembelea makatambuga na kuwpigia makofi na kuwalinda wasisemwe wala kuguswa! Haingii akilini kwakweli

Ni afadhali tungebaki chini ya mkoloni mweupe walau tungekuwa tumefika mbali miundombinu ingekuwa ya hali ya juu kuliko ilivo sasa, wageni wanachuma na kupeleka kwingine wakituacha kwenye ufukara, mashimo, vumbi. na giza tororo!
 
Kipindi hiki kuelekea 2010 utasikia mengi tu, kila mtu atajifanya mtetezi mkubwa wa wananchi.
 
Junius, umesema kweli. Mimi sioni umuhimu wa kelele zote hizi na pia sio mara ya kwanza wabunge kuzinduka usingizini zikifika nyakati kama hizi. Sioni kipya hapa, tulishsikia kelele nyingi huko nyuma kuhusu TRA, ATCL,TRL,TICTS, nchi inauzwa kwa wageni, mikataba mibovu n.k. Ni steps gani serikali imechukua ku-address issues hizi? Kinachonishangaza ni pale wabunge wanapopambana na miswada mbali, mbali bungeni utasikia sikubliani na hiki au kile halafu anapopmalizia kung'aka anamalizia kwa kusema anakubaliana na hoja hata kabla hajajibiwa! Aren't they all sick?
 
Wanataka ref wakirudi majimboni 2010....kwani wao hawakuwepo wakati mikataba mibovu inapitishwa kila mwaka Bunge lipo waliwahi kukwamishaa???hakuna jipya hapo....huyo selelii atapewa unaibu waziri nae atatulia yu wapi Njelu na G55?
 
wa-TZ tumezidi kuwa makondoo,yatesemwa mengi tu huko bungeni lakini mwisho wa siku hakuna kitakachofanyika afu watakuja kuomba kura tutawapa,hivi huu ujinga wetu utaisha lini? TUAMKE
 
Wanajua kuwa wakati huu ndio wa kuanza kushawishi wapiga kura kuendelea kuwachagua. Na kipindi hiki hata wabunge hao wasemeje, hawataambiwa chochote. Ni kipindi cha kukata mzizi wa fitna katika siasa.

Ukweli ni kwamba wanajua kuwa 2010 kura nyingi za CCM zitawaponyoka. Hivo kila mwenye uwezo wa kuzing'ang'ania anaanza sasa. Hakuna lolote zaidi ya propaganda tu hapo.
 
Kipindi hiki kuelekea 2010 utasikia mengi tu, kila mtu atajifanya mtetezi mkubwa wa wananchi.

Unachoongea ni sawa, kuna thread ilikuwepo humu inayosema utabiri wa mwalimu JK Nyerere ni kama aliyatabiri haya, tatizo lake hapa tulipofikia tunashindwa kujua yupi mkweli na yupi anatetea tumbo lake! maana naamini wote wapo wanaotetea ugali na wenye uchungu na nchi.
Sasa sijui itakuwaje!!?? Eee Mungu tuokoe na serikali hii inayo sababisha haya kwa kushindwa kutimiza wajibu wake!
 
Hawa Wabunge wasidanganye wapiga kura kwani kila kikao ni kuzungumzia mikataba ya kifisadi k.m. TICTS, madini, TRL, au mkataba wa ukodishaji wa KIA kwa chini ya dola tatu kwa siku ($1000 kwa mwaka), pasipo hatua yo yote kuchukuliwa.

Tutaona hata hiyo bajeti ikapita kwa NDIYOOOOOO.
 
uchaguzi unakaribia kila mbunge atakuwa "machachari"
 
Waziri mkuu ana kuwepo kwenye cabinet meetings. Raisi mwenyewe ndiyo bosi wa baraza la mawaziri. Kwa hiyo hamna kinacho weza kutendeka hawa waseme hawajui kitu. Wakisema hawajui kitu basi ina maana hawafanyi kazi yao ipaswavyo.

Naomba tujenge hoja zetu hapa, kama viongozi wote wakuu wanakuwepo ni dhahiri kuwa watu wanaoweza kutusaidia ni wabunge peke yao kwa kuiagiza serikali.

Mfumo wa bunge letu kuomba kila kitu ndicho chanzo cha maelekezo ya kamati ya bunge kuhusu Richmondi hayatekelezwe na spika anona sawa tu. Waziri mkuu anapiga porojo kila kiako cha bunge kinapofika na wabunge hawatambui kuwa wanadharauliwa.

Kama bungelimeshindwa kazi kwetu wapiga kura kuamua waendelee au la.
 
Mawaziri hawana uzalendo -Mbunge

*Adai ndio wanaiyumbisha nchi
*Wahusika Richmond waadhibiwe
*Apeleka ombi maalum kwa Pinda


Na John Daniel, Dodoma

MAWAZIRI wa Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete wamedaiwa kuiyumbisha nchi kutokana na mikataba mibovu wanayoingia ambayo hupitiwa na kuhakikiwa na watalaamu wao.

Akichangia hotuba ya bajeti bungeni jana, Mbunge wa Maswa, Bw. John Shibuda (CCM) alieleza kushangazwa na kukithiri mikataba mibovu inayoumiza taifa na wananchi hali inayozua shaka kuhusu uzalendo wa mawaziri hao.

Alisema kutokana na udhaifu huo, Watanzania wameshindwa kutambua uzalendo mawaziri kwani ndicho chombo cha juu kinachopitisha mikataba yote baada ya kuandaliwa na wataalamu wao lakini imejaa utata.


“TRC (Shirika la Reli Tanzania) lilikuwa na uongozi mzuri, tukachukua tukawapa watu
ambao hawana uwezo! Hivi sisi tutashika lini hatamu za nchi yetu?, Naomba mawaziri
mtusaidie mnatupeleka wapi?”Alihoji Bw.Shibuda na kuongeza;

“Mawaziri watujibu ni lini tutawapeleka Mahakama ya Kimataifa wawekezaji
wanaotunyonya, kila siku mikataba mibovu? Baraza la Mawaziri ndio wanapitisha
mikataba, Baraza la Mawaziri mnatarajia nini kipimo cha uzalendo wenu?” Alihoji
Mbunge huyo.


Alisema Serikali inakosa mapato kutokana na nchi kuingia mikataba mibovu hivyo kuwazidishia maisha magumu Watanzania huku dira ya maendeleo ikiwasahau wakulima na wafugaji bila kuwaandalia mazingira mazuri ya kuwainua kutokana na kile walicho nacho.

Kuhusu vitambulisho vya taifa, alisema ni jambo muhimu ambalo lingesaidia Serikali kukusanya mapato kwa urahisi zaidi lakini alisema mradi huo sasa umejaa ubinafsi na malumbano.

“Namwomba Waziri Mkuu aondoe kazi ya kutengeneza vitambulisho katika Wizara ya Mambo ya Ndani, kinachoendelea pale ni malumbano tu, tusibebane, uongozi wa kubebana umepitwa na wakati, kama mtu anataka yeye ndiye aonekane atupishe!”alisema Bw.Shibuda bila kufafanua kwa kina.

Kwa upande wake Mbunge wa Kishapu, Bw. Fredy Mpendazoe (CCM) aliitaka Serikali kujibu maswali manne mazito ya Watanzania ambayo ni muhimu kwa mustakali wa maendeleo ya nchi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti Watanzania wanataka majibu ya maswali yafuatayo “ Waliosaini
mikataba mibovu wamechukuliwa hatua gani? Wahusika wa mikataba ya TRL, mgodi wa Kiwira na Richmond wamechukuliwa hatua gani?”Alihoji na kuongeza;

“Ukitaka kumfukuza nzi tupa mzoga, Serikali kushindwa kuwachukulia hatua waovu ni kubariki uovu, penye uhuru ni pale watu wanapoweza kutoa maoni yao, ila penye demokrasia ni pale Serikali inaposikiliza maoni ya wananchi,”alisema Bw. Mpendazoe na kusisitiza kutaka Serikali itoe majibu ya maswali hayo.

Aliendelea “Serikali inayo wajibu wa kusikiliza maoni ya wananchi walioichagua.
Serikali haikuchaguliwa na malaika wala miungu bali ilichaguliwa na wananchi hivyo wana kila sababu ya kuikosoa,”alisisitiza Mbunge huyo


Bw. Mpendazoe alieleza kukerwa na tabia ya baadhi ya watu wanakejeli tatizo la ufisadi na kuita ni 'ajenda moja tu.'Aliwakosoa watu hao kwa msemo kwamba 'mawe yaliyochini ya bahari hayawezi kusikia kilio cha mtende ulio jangwani'.

Kuhusu DECI Mbunge huyo, alisema Serikali inapaswa kubeba msalaba wa wananchi wake
kujiunga na Kampuni hiyo inayodaiwa kuwa haramu kwani hawakuwa na namna yoyote ya kujipatia mitaji kutokana na kukosekana taratibu nzuri za kuinua mapato yao na kuondokana na umasikini.


Alisema DECI ni dalili ya wananchi kukata tamaa na kwamba sh. bilioni moja
zilizotolewa kwa ajili ya wajasiria mali na Rais Kikwete, hazikuwafikia walengwa kwa madai kwamba hawakidhi vigezo vya kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS).

Kuhusu ajira, Mbunge huyo alihoji Serikali kuhusu Wachina na Wakorea kujazana
Soko la Kuu la Kariakoo Dar es Salaam kufanya biashara ambazo zingefanywa na
Watanzania.

Alilalamikia pia kitendo cha Wakenya kuajiriwa na hoteli kubwa hapa nchini wakati Watanzania wanazo sifa na uwezo wa kufanya kazi hizo na kuhoji watu
hao wanapoingia Serikali haiwaoni?

Bw. Mpendazoe aligoma kuunga mkono hoja ya bajeti hiyo na kuahidi kufanya hivyo baada ya kujibiwa hoja zake.

Kwa upande wake Mbunge wa Mkanyageni Bw. Mohamed Habib Mnyaa (CUF), aliitaka Serikali kueleza sababu zilizosabaisha Shirika la madini ( STAMICO) kupewa kibali cha kukopa pesa Benki ya NBC tangu mwaka 2007 ili kununua mashine za kuchambua madini.

Alisema kitendo hicho ni ishara kwamba Serikali haitaki kuwaendeleza wazawa katika sekta hiyo na kwamba inawapa nafasi kubwa wawekezaji wa nje kuendelea kuvuna jasho la Watanzania.
 
uchaguzi unakaribia kila mbunge atakuwa "machachari"

mimi nadhani wanastahili pongezi kwasababu wamethubutu, pamoja na mapungufu yao (kukaa kimya) lakini sasa wamethubutu kusema maneno yenye maana. Hivi wangebaki kimya ingekuwa kwa faida ya nani? sasa wanasema kwa faida yao na walalahoi pia. Kudos Shibuda, Selelii nk
 
Date::6/22/2009
Bunge lamwagiza CAG azikague Meremeta, Tangold

Ramadhan Semtawa, Dodoma
Mwananchi

HATIMAYE Bunge limempa rungu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya uchunguzi maalumu kuhusu uwekezaji wa serikali kwenye makampuni tata ya Buhemba Goldmine (Meremeta) na Tangold, ambayo yamekuwa na tuhuma nzito za ufisadi.

Awali, CAG alizuiwa kukagua makampuni hayo kwa maelezo kuwa, kampuni ya Meremeta ni nyeti kwa kuwa ina uhusiano na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Habari zinasema kuwa, maagizo hayo yamo kwenye barua yenye kumbukumbu BC.50/155/06/98, ambayo katibu wa Bunge alimwandikia CAG Juni 8 mwaka huu akimtaka kufanya ukaguzi wa hesabu na thamani ya hisa na mtaji wa serikali katika makampuni hayo mawili.


Barua hiyo inamtaka CAG afanye ukaguzi maalumu ili kubaini thamani ya mtaji na hisa za serikali katika makampuni hayo tata na pia aieleze kamati kwa nini makampuni hayo hayakaguliwi.

Alipoulizwa kuhusu maagizo hayo, mkaguzi huyo mkuu wa serikali, Ludovick Utouh, alisema: ``Ni kweli nimepata barua ya bunge ikinitaka nifanye hivyo, lakini kueleza nitaanza lini na kumaliza lini, hapo brother nakuwa sina jibu la haraka."

Utouh alisisitiza kuwa hajapanga ataanza lini kazi hiyo akisema, "kupata barua na kuanza kazi ni vitu viwili tofauti."

Wakati Utouh akikiri kupata barua ya Bunge inayomtaka kukagua makampuni hayo, habari za kuaminika, ambazo zimethibitishwa na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, zinasema uamuzi huo ulitokana na msimamo wa kamati hiyo kutaka hesabu za makampuni hayo ambayo serikali ina hisa, yakaguliwe.

Suala la Meremeta na Tangold linaweza kutolewa maelezo na serikali leo baada ya mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Wilbrod Slaa kuhoji sababu za serikali kusitasita kuzifanyia ukaguzi hata pale wananchi walipoonyesha wasiwasi wao wa kuwepo kwa ufisadi.

Suala hilo pia linaweza kuibuka wakati wa hotuba mbadala ya kambi ya upinzani ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo huenda ikasomwa na Dk Slaa.

Alipoulizwa kuhusu maagizo hayo, Zitto alijibu: "Kumekuwa na kelele nyingi kuhusu Meremeta na Tangold, lakini serikali haichukui hatua na hivyo hatufiki mwisho.


"Kamati yangu imeamua kufanya uchunguzi huo na tayari CAG amekwishaanza kazi hiyo. Lazima ifike wakati tufunge mijadala hii ili nchi ifanye mambo mengine.

"Nimeagiza uchunguzi maalumu wa Meremeta tangu Juni 8. Mimi si mtu wa kusema tu, natenda na kutimiza wajibu wangu."

Zitto alifafanua kwamba Kamati ya Jaji Bomani iliagiza uchunguzi wa kina dhidi ya makampuni hayo na kwamba, "baada ya CAG, kamati itawasilisha bungeni ripoti maalumu ya Meremeta ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya yeyote atakayehusika na upotevu ule wa pesa Sh155 bilioni."

Utata mkubwa uliopo Meremeta ambayo inamiliki mgodi wa dhahabu wa Buhemba, pamoja na tuhuma za ufisadi ni kuhusu wanahisa.

Serikali imekuwa ikijitetea kuwa kampuni hiyo inahusu masuala ya ulinzi na usalama wa nchi, hivyo si vema kuanika hadharani shughuli zake.
 
Back
Top Bottom