John Terry Vs Nemanja Vidic, nani alikuwa zaidi?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Hawa wote walikuwa ni mabeki wa kati. Pia wote walikuwa ni makepteni katika timu zao.
Wakati John Terry alikipiga Chelsea, Nemanja Vidic alikipiga Man United katika EPL.

Kwasasa wote wameshastaafu, ukiwa kama mshabiki wa mpira, ni beki gani kati ya hao wawili ambaye ulimkubali zaidi kwa uchezaji wake akiwa uwanjani.

Karibuni kwa mjadala.
 
Hawa wote walikuwa wana uchezaji wa aina moja, yaani lazima mtu afie uwanjani. Ila mimi namkubali Terry bana yule hata ulikuwa ukitema mate anayakaba.
 
Kwangu mimi Nemanja Vidic ni bora zaidi.

Kwanza ndio beki pekee kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa EPL mara mbili.

Licha ya ufanano wa aina yao ya uchezaji, Captain Nemanja Vidic anabakia kuwa beki kisiki, mahiri na anayrjitolea kwa 100% kuhakikisha timu yake inakuwa salama. Muulize Didier Drogba, anafahamu vyema habari za Vidic.
 
Vida ni habari isiyo ya kawaida. Anakupa dimension tofauti ukitaka ustaarabu sawa,ubabe sawa,uhuni sawa. Yaani anakupa unachokitaka na kinachohitajika. Terry labda afananishwe na Rio Ferdinand na bado mnyukano hapo ni mkali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…