Johnson Mashaka na mbio za Ubunge Ukonga

hiyo bold inaonyesha kuwa yote uliyoyaandika ni uwongo
 
Huko bungeni kuna nini hasa mpaka mtu atenge $.350,000 kwa ajili ya kampeni. Kwa nini mtu hasitoe msaada tu mpaka uingie bungeni. Siamini kama habari hizi ni za kweli na kama ni za kweli basi hata huyo Mashaka atakuwa BONGOLALA tu.

Hata kama hawa vijana wakiamua kugombea (Mashaka, Shayo na January Makamba) ndani ya SISIEMU ni UPUPU tu. Ukishaingia SISIEMU basi umeliwa. Mfano ni Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na Madini na Nishati. Hao ni vijana ambao tuliona wangeweza kuleta mabadiliko nchini. Lakini ndimi zao zote ni za kifisadifisadi tu. Wanaimba nyimbo zilezile za Chimwaga tu.
 
Aibu ya karne itatukumba wana Jamii Forums pale itakapojulikana kwamba bwana mdogo wala hakuwa na nia ya kugombea Ubunge....

Si kweli;JF haitakumbwa na aibu kamwe hata kama Kijana John Mashaka atamua kugombea Ubunge wa jimbo a Ukonga maana atashindwa vibaya mno kwa sababu HANA MTAJI WA WATU;hata aje na dola milion 1 hazitabadili matokeo!

Mimi binafsi na wenzangu wakazi wa Kitunda,huwa tunamuona Kijana Johm Mashaka kwenye TV na kwenye blog ya Michuzi ambayo inamtangaza kweli kweli kila kukicha;huwezi kupata kura za wana Ukonga kwa vile tu unaonekana kwenye media ukiongeaa kimombo!

Kuhusu makazi ya kijana huyu;kama bado hajahama;basi John Mashaka bado anaishi North Carolina,akiwa mfanyakazi wa moja ya matawi mengi ya Bank ya Wachovia mjini Charlotte,na rafiki zake wakubwa kule ni pamoja na mzee mmoja Mtanzania mchungaji wa kanisa.

John Mashaka hajawahi kufanya kazi mji wowote wa Texas na habari zilizoenezwa kuwa John Masha ni mmoja wa maafisa wa bank za USA pale Wall Street waliopewa kazi ya kuufufua uchumi uliodorora wa Marekani HAZINA UKWELI WOWOTE!

Ukonga ni kwa wana Ukonga,na kamwe hela haziwezi kukupa Ubunge wa Ukonga!
 
Aibu ya karne itatukumba wana Jamii Forums pale itakapojulikana kwamba bwana mdogo wala hakuwa na nia ya kugombea Ubunge....

Watu wana uzushi wa ajabu sana hapa, kuna watu wana a voyeuristic fascination with alternate history and the branching universe theory kiasi wanaweza kukwambia mambo ya ajabu ili mradi wachekelee reaction ya watu itakavyokuwa humu ndani na mjadala utakavyoendelea.There oughta be rules to substantially prove your case before presenting half baked rumors here.
 
Huyu Nape wako hafui dafu kwa Myika huko Ubungo afadhali angekwenda Temeke anaweza kuambulia!! Ubungo wamejaa wasomi wasioweza kurubuniwa na propaganda za CCM!!Kama Nape haamini ajaribu aone atakavyogaragazwa.
Mkuu, marekebisho kidogo tu.

Kinyume cha uliyoyasema ndio kweli, endapo Nape atashinda kwa ticket ya CCM (yeyote atakaeshinda kwa CCM atamshinda yeyote atakaekwenda kule). Mimi sio mwamuzi ila ndivyo Jimbo lilivyo kwa sasa. Tutaona 2010. Nakuombea afya njema kushuhudia hili.
 
Kwa kuongezea tu Mkuu. Kata nyingine ni Chanika.
Masahihisho: Amekaa Bungeni miaka 10 akiwa Mbunge wa Ukonga. Kati ya hiyo, ni miaka minne tu ndio amekuwa katika serikali.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…