MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 65
- 81
Aliyekuwa Mwanachama, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge kwa kipindi cha miaka 10 kupitia chama hicho ambaye hivi karibuni alirejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mchungaji Peter Msigwa amemshutumu Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kuanzisha foundation yake (Mbowe Foundation) ingali akiwa madarakani hali inayoibua mgongano wa kimaslahi kama vile kwa sasa fedha na michango mbalimbali ya chama hicho inapitia kwenye akaunti ya foundation hiyo badala ya akaunti za chama.
Aidha amedai programu za Join the Chain na Chadema Digital zinamilikiwa na kampuni moja ya nchini Kenya ambayo Mwenyekiti Mbowe ni mbia. Kwa maelezo yake michango yote hiyo inaonekana inaishia mfukoni kwa Mbowe.
Shutuma hizi hazihitaji majibu mepesi mepesi.