Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
✳️ CHIMBUKO LA CHAMA CHA MAPINDUZI NI MASHINA; CDE JOKATE
🗓️ 04 Mei, 2024
📍Geita
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amesema Chimbuko la Chama cha Mapinduzi ni kutoka kwenye Mashina kwani huko ndipo kwenye Wanachama na Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi.
Ndugu Jokate ameyasema hayo wakati anaongea na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwenye Mkutano wa shina la CCM namba 5 Geita Mjini.
"Ndugu zangu Chimbuko la Chama cha Mapinduzi lipo huku kwenye Matawi, huku ndipo walipo Wanachama na Wakereketwa wote wa CCM, lazima huku tuje tuone maendeleo ya Wanachama wetu"
Aidha Katibu Mkuu Ndugu Jokate amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 utatoa Mwanga wa uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 hivyo ni lazima wana CCM kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa CCM Inashinda kwa Kishindo.
"Mwaka huu tuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi huu ni Muhimu sana kwetu kujitathmini kuelekea Uchaguzi mkuu wa 2025 hivyo ni lazima sisi Chama cha Mapinduzi tuhakikishe tumapata Uchindi wa Kutosha ambao utatupa mwanga wa Uchaguzi Mkuu 2025 ili tukamheshimishe Mwenyekiti wetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan".
"Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi ilishatoa msimamo kuhusu Uchaguzi Mkuu 2025 kuwa Fomu itatoka moja tu, hivyo ndugu zangu msibabaishwe na mitandao ya Kijamii, Sisi UVCCM Msimamo wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi Ndio Msimamo wetu".
#KulindaNaKujengaUjamaa
#SisiNaMamaMleziWaWana
#Kaziiendelee
Imetolewa na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-05-04 at 14.32.46.jpeg297.6 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 15.02.00.jpeg477.2 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 15.07.08.jpeg285 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 15.07.11.jpeg555.2 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 15.07.12.jpeg461.8 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 15.07.13(1).jpeg257.7 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 20.08.00.jpeg381.9 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 20.07.56.jpeg588.8 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 19.58.08.jpeg328 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 19.58.03.jpeg545.1 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-05-04 at 20.07.52.jpeg695.2 KB · Views: 5