Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amepokelewa katika ofisi za CCM Mkoa wa Njombe leo Novemba 26, 2024 kwa lengo la kufunga Kampeni Uchaguzi wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji zitakazofanyika Kata ya Ulembwe, Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani humo.
Baada ya Msafara wa mapokezi hayo; Ndugu Jokate alipata wasaa wa kuendesha kikao cha ndani kilichowakutanisha Viongozi wa CCM na Jumuiya zake wa Ngazi ya Mkoa na Wilaya pamoja na kupokea taarifa ya kazi.