Mwana kwanza una akili gani kwenda kwa mkewe? Kweli ulitaka ukamle uroda mke wake? Hapo tu inaonyesha una matatizo yako. Kama mchungaji ndiyo tabia yake una uhakika gani na afya ya mkewe? Na hata kama mkewe ni salama uumle uroda ili iweje? Mtu waku shugulika nae ni mkeo maana mkeo haja bakwa kakubali mwenyewe kumegwa haja lazimishwa. Nakushauri nenda na mkeo kama ni kwa mshenga au wazazi au yoyote yule mnaye muamini na swala hili mliongelee mjue muende wapi baada ya hapa. Pili, kama utaamua kubaki na mkeo, na mimi nasema kila mtu anastahili apewe nafasi ya pili, nakushauri mkapime. Mpime magonjwa yote ya zinaa pamoja na gonjwa kuu. Mwishoni nataka kusema lazima kuna sababu mkeo kaamua kwenda nje nakushauri uongee nae ujue hiyo sababu ni ipi ili mtatue kosa lisiji rudie. Mwishoni kabisa nataka kusema hili swala linataka utaratibu na busara. Nawatakia kila laheri.