Jokote Mwegelo: Msipandishe bei ya Vyakula

Jokote Mwegelo: Msipandishe bei ya Vyakula

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Jokate Mwegelo amewataka Wafanyabiashara Wilayani humo kutopandisha bei ya vyakula kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

DC Jokate ameyasema hayo tarehe 23 Machi, 2023 akiwa Ofisini kwake baada ya kumaliza kikao na Uongozi wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Wilayani Korogwe.

Jokate amesema kumekuwa na tabia ya Wafanyabiashara kuficha vyakula ili waweze kuongeza bei kwa kisingizio kwamba vyakula hivyo havipatikani sokoni ambapo amewataka Wafanyabiashara kuacha tabia hiyo kwani kufunga ni njia ya kumkaribia Mungu ”Msitumie nafasi hii ya Mwezi Mtukufu kuongeza bei ya vyakula”

DC Jokate pia amesema Korogwe ipo salama na chakula kipo cha kutosha Wilayani humo hivyo Wananchi wasiwe na mashaka juu ya hilo.

Katika hatua nyingine Jokate amewatakia Waislamu wote Wilayani Korogwe na Tanzania kwa ujumla Mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

WhatsApp Image 2023-03-24 at 00.21.00(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-24 at 00.21.00.jpeg
 
Jokate unaelewa maana ya kilimo ni biashara?unajua theory ya demand & supply,kilimo syo rahisi hivyo kama unavyodhani ni lazima watu waweke stock wafanya biashara wauze baadae bei ikiwa rafiki
 
Back
Top Bottom