Jonas Mkude: Kinachowaangamiza Simba ni kiburi, Jifunzeni kutokana na haya

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Inasemekana kwamba jitihada za Jonas Mkude kuongeza mkataba na klabu yake Simba SC upo kwenye utata mkubwa sana.

Inaonekana mkataba mpya wa Jonas Mkude unadai alipwe fedha zaidi ambazo amekuwa akilipwa kipindi aongezapo mkataba.

Hili suala la ongezeko la pesa za kusaini mkataba mpya limefanya viongozi wa simba sc kumuona kama mchezaji huyo ni msaliti na kuwa hana mapenzi na timu hiyo ambayo imemlea tangu ujana wake.

Hanspope alionekana kulalamika kwenye moja ya chombo cha Habari kuwa haiwezekani mchezaji waliomlea na kumkuza wao wenyewe atake kiasi kikubwa cha pesa ili aongeze mkataba.

"Kama ataki kucheza simba basi aende huko Yanga SC ambapo watamlipa hizo pesa... Mchezaji amejaa tamaa ya pesa sana" Alisema Hans Pope

.................................................................................

Simba ndio mnao haribu soka la Bongo. Mnasindwa kujua kuwa sasa ni wakati wa kubadilisha soka kutoka la Burudani kuwa la kulipwa..

Kumbukeni kuwa hawa vijana hawana kazi, wameamua kufanya soka kuwa ni kazi. Inapaswa kazi yao iheshimiwe kama kazi yako wewe inavyoheshimika....

Yule ni mchezaji wa kumtegemea sana kwenye kikosi chenu kwa sasa (zaidi ya kichuya) cha kushangaza mnamchukulia kama kapuku fulani hivi... Yaani iweje Mavugo alipwe pesa ndefu zaidi yake.. Ukizingatia yeye ndiyo mwenye kiwango zaidi ya huyo Mavugo.

Igeni waingereza pale. Ona salary ya Rooney! Kipindi anafanyiwa salary increment yeye ndiye alikuwa dependable player.

Huwa mnajifanya viburi sana. Eti ohh acha aende simba ni kubwa kuliko yeye. Hilo si sawa kabisa.

Inaonekana bado hamjajifunza mpaka leo.

1. Tangu Yondani asepe hamkuwahi pata mlinzi mwenye hadhi yake....

2. Tangu Tambwe asepe hamjawahi pata striker mwenye hadhi yake na ubora wake.

3. Tangu Messi "Singano" asepe hamjawahi pata winga wa kulia mwenye uwezo kama yeye (licha ya kuwa Kichuya anajaribu kuwasahaulisha....

4. Tangu Kessy asepe hamjafanikiwa kumpata mbadala wa huyu kijana. (Mnatudanganya kuwa Bokungu ameweza)

5. Tangu akina Barthez na Dida wasepe pale hamjawahi pata walinda milango wenye ubora sawa na wakudumu kwa kitambo kirefu....

Simba acheni kiburi cha kujiona kuwa mnauwezo wa kuwaacha wachezaji wenu muhimu na kujidai kuwa mna uwezo mzuri wa kuwa replace.
 
Daaa kweli inabd wabadilike aisee

Sent from mTalk
 
Hatuhitaji ushauri wa kunyenyekea wachezaji. Wachezaji ni kama wafanyakazi wengine na wana wajibu wa kutimiza majukumu yao.Wana wakala ambao ndio wataongea na klabu kwa niaba yao.Mchezaji anayejithamini na kujua wajibu wake haropoki hovyo bali huwa anaacha kazi za kuboreshwa mkataba wake kwa wakala. Simba hatujazoea kupiga magoti kazi hiyo inafanywa na timu zinazokubali kuwa blackmailed na wachezaji wasiojua wajibu wao.
 
Hatuhitaji ushauri wa kunyenyekea wachezaji. Wachezaji ni kama wafanyakazi wengine na wana wajibu wa kutimiza majukumu yao..

Kutimiza majukumu gani hayo! Hamjui kuwa mpira ni kazi kama kazi nyingine...?

Kwa maana yako... Atimize majukumu ya kuchezea Simba hata kama haina uwezo(au haitaku kumlipa maslahi anayotaka mchezaji)? si ndio?
 
Kama Hans alisema huu upuuuzi basi naunga mkono Mkude aende tu Yanga.
 
Simba hatujazoea kupiga magoti kazi hiyo inafanywa na timu zinazokubali kuwa blackmailed na wachezaji wasiojua wajibu wao.

Matunda ya unachokisema ni simba sc kushindwa kutwaa ubingwa wa ligi kwa miaka 5 mfululizo......

Mkiendelea kujifanya viburi mtasikiaga ubingwa tu kupitia kwenye Bomba!

Muacheni sasa huyo... Muone mtakavyo isoma namba...
 

Uko sahihi kabisa Mkuu.. Simba in kubwa zaidi ya Mkude.
 
Majukumu ya kucheza mpira na kufanya mazoezi. Hakuna mchezaji analazimishwa. Ndio maana Yanga walishindwana na Kavumbangu na Domayo wakaenda Azam.Hilo ni jambo la kawaida. Sasa hivi Lingard anataka aongezewe mshahara na Man United lakini humsikii akisema naenda Liverpool nisipopata mshahara ninaoutaka,bali wakala ndio anadeal na mazungumzo. Mwaka 2014 Yanga walitaka kumsajili Mkude kwa milioni 80 akawazimia simu nalo pia ni kosa la Yanga. Inaelekea unaipenda Simba kisiri kwa sababu kwanini ikuume tukiacha mchezaji?Juhudi zako hizo ukizielekeza kwenye kutatua matatizo ya timu yako kumilikiwa kinguvu na mtu mmoja.Akitishia kuondoka mnapigia magoti na rasilimali nyingi tu mnazo.
 
Messi mwenyewe kalelewa na Barcelona na bado anawadindia kusaini mkataba mpaka waongeze hela na wanaelewa, sembuse hizi hela za madafu hapa!
 
Real Madrid hajatwaa ubingwa tokea 2012 nae ameacha wachezaji?Mijitu mengine unashangaa wanafikiri kwa kutumia nini?Liverpool leo ni mwaka wa 25 hawajatwaa ubingwa.Cha ajabu nini?Yanga mlipokuwa na maamuzi ya pamoja mlifukuza timu nzima ikisheheni wachezaji wa maana. Mtaanza upya. Leo hamna ubavu wa kuacha mchezaji hata akidengua kwa sababu timu yenu leo inamilikiwa na mtu mmoja ukipinga unafutwa unachama.Kama wewe ni mwanachama pinga uone. Dr.Tiboroha alijaribu leo yupo Stendi United.
 
Sijawahi kusikia mchezaji kutoka yanga kwenda simba yeye aondoke tu
 
Kutimiza majukumu gani hayo! Hamjui kuwa mpira ni kazi kama kazi nyingine...?

Kwa maana yako... Atimize majukumu ya kuchezea Simba hata kama haina uwezo(au haitaku kumlipa maslahi anayotaka mchezaji)? si ndio?
Maslahi gani...? ya mchezaji kutaka kiwango kikubwa kama ndo anasajiliwa ilhali ni kuongeza tu mkataba..!? hakuna kitu kama hicho, aende tu huku vyura FC
 
Acha kuchanganya mambo mkuu..Barthez na Dida si masuala ya mikataba

Hawa nafasi yao ilikuwa finyu kwa sababu ya Kaseja na Tambwe alionekana kama kiwango kimeshuka

Wewe kuna uliko egemea ndo maana unachanganya maslahi, mikataba, kushuka kiwango

aende tu Simba itakuwapo tu..!
 
Messi mwenyewe kalelewa na Barcelona na bado anawadindia kusaini mkataba mpaka waongeze hela na wanaelewa, sembuse hizi hela za madafu hapa!
Yaani ndio hapo Mkuu..

Hawa wabongo wa mtaa wa Msimbazi pale wanapenda vya bure sanaa....

Wanataka cha uvunguni lakini cha ajabu hawataki kuinama....

Sasa ona mtu kama Messi hapo... [emoji23]
 
Sijawahi kusikia mchezaji kutoka yanga kwenda simba yeye aondoke tu
Huwezi kusikia hilo suala kwenye Karne hii... Ukizingatiza tabia ya hawa Jamaa wa Simba dhidi ya wachezaji wao....

Hata hivyo! Pale wanacheza tu... Ila wanamalengo ya kuichezea Yanga kwa ajili ya Mafanikio...

Ndio maana wengi wakiwa kwenye form pale simba hupenda sana kukimbilia Yanga ambapo wanajua kuwa ni mahala pekee ambapo mchezaji unaweza pata Mafanikio...
 

Jeuri ya bure tu, akiondoka Hamna mtu wa kuziba nafasi Yake na ndio mtapotea mazima!
Ni Haki yake kuomba nyongeza ya mshahara kwa sababu hata ubora wa kazi yake unaonekana
 
Hujakosea.

Ila ukisoma vizuri utajua Udhui kuu la Uzi.

Iwe Kiwango, Mkataba au Bifu baina ya Mchezaji na kiongozi. Hili suala limewafanya mkose mengi sana haswa mafanikia kwenye hii miaka ya karibuni....

Kaseja alipokuwa namba one golini, nani alikiwa kipa namba 2 au 3...?

Ina maana akina Dida na Barthez walikuwa na kiwango cha chini sana hata wakose sifa za kuitwa golikipa namba 2 au 3..?

Tatizo nyie mna majivuni mengi sana..

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…