Joob na kibwa na shomari waongezewe mshahara

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Shalom! Shaom! Baada ya salaam niende moja kwa moja kwenye pointi Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza .

Natuma ujumbe huu kwa viongozi wa yanga walitizame hili na walifanyie kazi haraka iwezekanavyo.

Ndiyoooo vijana wetu wanapiga kazi kubwa sana nakujituma ndani ya timu mpaka kazi inaonekana

Hakuna asiyejua kazi ya beki mwenye akili jobu aka the big brain defender Kama tulivyombatiza mashabiki.

Hakika jobu ni kisiki haswaaa ni muda wa yanga kumuongeza bonus na mshahara huyu mwamba kwani nitasikitika sana ikiwa wachezaji wakigeni wakilipwa vizuri lakini jobu na kibwana wakipewa mshahara kichele.

Kibwana shomari ni kiraka anayecheza mbavu ya kushoto nakulia na kitasa mbishi hakuna mwanayanga asiyejua umuhimu wa kibwana shomari.

Nikiwa Kama shabiki wa yanga ninayeipenda yanga na ni mwanachama hai wa yanga,
Yanga boresheni mishahara ya hawa wazawa hakika kazi zao tunaziona zinatufurahisha kweli kweli.

Ndiyoooo Kama analipwa vizuri morison kwa Nini msiboreshe mishahara ya wazawa ili isije kutokea ya feisal maana kilichotokea kwa feisal ni funzo tosha.
 
Moderaters weka vizuri kichwa Cha habari.
 
umeongea Utumbo mtupu,umeiona mikataba yao......uzuri ulichokiongea ni maoni sio maagizo,hakuna mtu atakusikiliza wewe mpumbavu kolo
 
Tulia unapoandika..
Haraka ya wap hyo
 
Kweni sasa hivi wanalipwa kiasi gani mpaka uone hakiwatoshi?

Wamekwambia kwamba hakiwatoshi?

Umejuaje je kama yapo mazungumzo yanaendelea ya kuwaongezea mshahara?
 
Waongezewe mishahara toka kiasi hadi kiasi gani?
Wao wenyewe ni watoto wadogo hawawezi kuongea na waajiri wao kama ela waongezewe mpaka uje uwaongelee wewe kama nani?
Kwanini uje uongelee humu, kwanini usiende ofisi za Yanga kukutana na waajili wao ili uongee kama umetumwa au ni wakala wao?
 
Ishu ni wao wenyewe kwenye mikataba yao sio viongozi waongeze pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…