Movic Evara
Senior Member
- Jan 31, 2018
- 197
- 431
Uchaguzi wa bunge la ulaya umemalizika jana kwa raia kutoka nchi 27 kupiga kura kuchagua wabunge watakaowawakilisha katika bunge la ulaya ambapo vyama vya siasa vya mrengo wa kulia vimeonekana kufanya vizuri.
Nchini ufaransa, chama cha mrengo wa kulia cha “National Rally, NR” kimefanya vizuri zaidi kwa kupata asilimia 32 ya kura na kukizidi chama anachotoka rais Emmmanel Macron, Renaissance, kilichopata asilimia 15 ya kura.
Kijana mdogo, umri miaka 28 amemuweka roho juu rais Macron. Namzungumzia Jordan Bardella rais wa sasa wa chama cha National Rally ambaye ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na kuendelea kutetea kiti chake katika bunge la ulaya.
Ushindi wa chama cha National Rally hauaathiri chochote ndani ya Ufaransa kwa sasa, lakini unaleta ishara kwenye siasa za ndani ya Ufaransa. Ishara kwamba wananchi wamepoteza imani na chama cha Renaissance anachotoka Rais Macron.
Rais Macron ameingia hofu. Ameona dalili za chama cha mrengo wa kulia, NR kuzidi kuimarika kupendwa na wananchi. Ameona wabunge wa chama chake wamekosa mvuto kwa wananchi.
Hivyo ameamua kuvunja bunge na kutangaza kufanyika kwa uchaguzi wa mapema ili wananchi wachague wabunge wengine sahihi. Anaamini wananchi watachagua wabunge wengi (zaidi ya 289) kutoka chama chake, Renaissance.
Hapa Macron amecheza Kamari. Kwani ana uhakika gani kama chama chake kitashinda kwa kupata viti vingi? Je, vipi kama wananchi watachagua wabunge wengi kutoka chama cha National Rally na kukipa ushindi wa viti vingi bungeni? Vipi chama cha Renaissance kikishindwa kudhibiti bunge kwa mara nyingine?
Endapo uchaguzi utafanyika na chama cha Renaissance kitashindwa kupata kura za kutosha, basi Macron atalazimika kufanya kitu kinaitwa ‘Cohabitation’ ambapo Waziri mkuu atachaguliwa kutoka chama cha upinzani ili kuhirikiana na rais katika kuongoza serikali.
Hiyo inanitukumbusha mwaka 1997 ambapo rais wa Ufaransa, Jacques Chirac alicheza kamari ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema akitegemea kupata wabunge wengi zaidi. Lakini matokeo yakaja kinyume chake. Chama chake cha PRP kikapoteza viti vingi kuliko ilivyokuwa navyo mwanzo. Hiyo ilimfanya waziri mkuu, ateuliwe kutoka chama cha upinzani cha Socialist Party SP. Ndipo akachaguliwa Lionel Jospin kuwa waziri mkuu.
Tukio hilo la mwaka 1997 ni funzo la sasa kwa Macron. Ameitisha uchaguzi tarehe 30 Juni. Ikitokea chama chake kikashindwa kupata kura 289, atalazimika kufanya Cohabitation. Maana yake, Waziri mkuu atatoka chama cha upinzani chenye nguvu. Unadhani ni chama gani hiko kama sio National Rally, NR?
Na endapo 'National Rally' watatoa Waziri mkuu, unadhani ni nani mwingine ataweza kuteuliwa kuwa Waziri mkuu kama sio kijana mdogo wa miaka 28, Jordan Bardella aliyetokea kupendwa na kuaminiwa na raia wengi wa ufaransa?
Bila shaka Jordan Bardella ni tishio kwa Rais Emmanuel Macron. Kijana Bardella ni zao la mwanasiasa mkongwe bi Marine Le Pen. Bi Marie Le Pen ni mwanamama aliyegombea urais kwenye chaguzi za mwaka 2012, 2017, 2022 akiongoza chama cha National Rally tangu mwaka 2011 hadi 2022 alipomwachia kijana Bardella.
Kwa sasa Bi Marine Le Pen ni mbunge na kiongozi wa chama cha National Rally bungeni. Baba yake, aitwaye Jean Marie Le Pen ndiye mwanzilishi na kiongozi wa chama hiki cha Rally kuanzia mwaka 1972 hadi 2011.
Naomba kuishia hapa.
Imeandikwa na
©️KichwaKikuu.