Jorge Vilda ameshambuliwa vikali na wadau wa soka baada ya kuonekana akimshika vibaya kocha wa kike

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Meneja wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Hispania, Jorge Vilda ameshambuliwa vikali na wadau wa soka baada ya kuonekana akimshika vibaya kocha wa kike wakati wa kusheherekea ushindi wa Kombe la Dunia la Wanawake 2023.

Video ya sekunde 10 iliyosambaa mitandaoni imemuonyesha Meneja huyo akimshika kifuani mfanyakazi wa kike wa timu hiyo kwa namna isiyofaa.

Vilda ambaye ni mchezaji wa zamani wa Real Madrid amekuwa akilalamikiwa na wachezaji wa zamani na wa sasa kwa tabia mbalimbali ambazo zisizofaa.

Tukio hilo limeongeza hasira na wasiwasi kwa mashabiki na wadau wa soka nchini Hispania ambao mara kwa mara wamekuwa wakichukizwa na tabia za Meneja huyo.

Itakumbukwa kuwa wadau mbalimbali bado wanafuatilia hatima ya kitendo cha Rais wa Shirikisho la soka la Hispania Luis Rubiales kumpiga busu mdomoni mchezaji wa kike Jenni Hermoso juzi wakati wa kusheherekea ushindi wa kombe la dunia.


 
Mbona kocha anachekelea hapo wala hajashituka, watakuwa wana pelekeana moto hao🤣
 
Hata hizi academy uchwara za huku mtaani hayo ni ya kawaida ila kwa sababh wale watoto wa kike wanaamini watatoka kimaisha wanaamua kukaa kimya licha ya kushikwashikwa
 
Soka lilikuwa ni la wanaume tu, na ndo inavyotakiwa, sasa nyinyi mlipoleta soka la wanawake mlikuwa mnatarajia nini? Tukiachana na hilo, huko Ulaya ambako watu wanakaa uchi uchi mnadhani wanastahili kutendewa kiungwana? Mimi mwenyewe ningewapiga finger sana tu.
 
Kuna mwingine wa spain naona kapiga denda kabisa huko 😄
 
Hata kibadeni alikuwa na tabia chafu kwa watoto wa kiume. Inaudhi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…