Jose Mourinho afutwa kazi Chelsea

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Posts
2,268
Reaction score
335


Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.

Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.

Chelsea walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 ligini kufikia sasa.

mechi ya mwisho kwa Mourinho kwenye usukani ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi Leicester City 2-1.

Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi.

Chanzo: BBC Swahili
 

Attachments

  • 151207054637_jose_mourinho_512x288_reuters.jpg
    15.9 KB · Views: 5,611
kocha wa chelsea jose morinho ametimuliwa kazi katika club hiyo ya jijini london
 
Jose " special one" Mourinho amefukuzwa kazi rasmi ikiwa ni miezi 7 tu tangu alipofanikiwa kutwaa ubingwa wa England Msimu huu.

Makocha wanaopewa nafasi kubwa kumrithi ni Pep Guadiola, Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos

Source: BBC Website 17:50 17.12.2015.
 
Duh! Anaondoka na 40mil pounds za fidia! Dah!
Ila Roman kweli hataki mchezo! Yee ukiboronga, lazima akupe teke kwenye kalio!
 
Duh! Anaondoka na 40mil pounds za fidia! Dah!
Ila Roman kweli hataki mchezo! Yee ukiboronga, lazima akupe teke kwenye kalio!

40 milion pound
halafu Real Madrid wanamtaka...life is unfair
 
Mourinho aende kulamba malimao , wazee wa darajani wamemchoka sasa.
 
kwangu ni heri chelsea tufungwe hata tushuke daraja kuliko kuondoka kwa Mou... imeniuma sana.... heri abaki...

aliichukua timu ikiwa ya kawaida sana akasaidia kuipandisha hadi pale ilifika... ikapata mashabiki kibao, ambao wengi wao tumekuwa wazalendo zaidi kwa Mourinho kuliko Chelsea halafu leo mnamfukuza??
 

Mourinho ndie alienipeleka Chelsea na nimeondoka Chelsea
 
Mourinho ndie alienipeleka Chelsea na nimeondoka Chelsea

mkuu ngoja tuone linalofuata.... labda linaweza kuja li Pep Guardiaola.... ila kokote atakakokuwa Mourinho nitahamia ku support hiyo timu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…