kwangu ni heri chelsea tufungwe hata tushuke daraja kuliko kuondoka kwa Mou... imeniuma sana.... heri abaki...
aliichukua timu ikiwa ya kawaida sana akasaidia kuipandisha hadi pale ilifika... ikapata mashabiki kibao, ambao wengi wao tumekuwa wazalendo zaidi kwa Mourinho kuliko Chelsea halafu leo mnamfukuza??
mkuu ucl amechukua mara 3 porto, inter, realAcha kumfananisha Mourinho na Wenger unajishushia heshima,
Mafanikio ya Mourinho Wenger ataendelea kuyaota ndotoni tu,
Tuchukulie UCL tu, Mourinho amechukua mara 2 akiwa na team za Porto na Chelsea,wenger Kombe la UCL atalisikia tu mpaka anastaafu,kwanza asubiri mziki wa Barcelona
Duh! Anaondoka na 40mil pounds za fidia! Dah!
Ila Roman kweli hataki mchezo! Yee ukiboronga, lazima akupe teke kwenye kalio!
40 milion pound
halafu Real Madrid wanamtaka...life is unfair
Mourinho huwa hamkejeli Wenger, anamwambiaga ukweli.
Unakumbuka aliwahi kumwambia kwamba kazi ya Wenger haina stress kwa sababu hawazi kufukuzwa hata kama matokeo ni mabaya.
Na Mou alisema ikitokea msimu ukaisha hajachukua kombe anafukuzwa au anaacha kazi, na ndicho kilichomtokea, wameona kwamba hatachukua kombe wakamfukuza. Wenger hata miaka kumi ipite no problem.
This time around Roman alikuwa makini sana. Atalipwa the rest of his salary kwa msimu huu tu. Then some other benefits. Sidhani kama itafika Pound million 15. All the same si haba!
Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.
Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.
Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.
Chelsea walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 ligini kufikia sasa.
mechi ya mwisho kwa Mourinho kwenye usukani ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi Leicester City 2-1.
Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi.
Chanzo: BBC Swahili
mkuu ucl amechukua mara 3 porto, inter, real
Kwaio msimu umeshaisha?
Utasubiri sana...hashuki mtu!Kwa sasa naomba Chelsea washuke daraja! Sina huruma nao tena, nilikuwa namuonea huruma Mourinho!
Na akienda Madrid aka perform itakuwa verry funny
kwangu ni heri chelsea tufungwe hata tushuke daraja kuliko kuondoka kwa Mou... imeniuma sana.... heri abaki...
aliichukua timu ikiwa ya kawaida sana akasaidia kuipandisha hadi pale ilifika... ikapata mashabiki kibao, ambao wengi wao tumekuwa wazalendo zaidi kwa Mourinho kuliko Chelsea halafu leo mnamfukuza??