Jose Mourinho akilalamikia kiwango cha fedha cha £300m alichopewa kununua wachezaji kuwa hakitoshi

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa kiwango cha fedha cha £300m alichopewa kununua wachezaji kuimarisha kikosi chake hakitoshi.

"Tuko katika mwaka wa pili kujaribu kujenga timu ambayo unajua sio miongoni mwa timu bora duniani", alisema kocha huyo raia wa Ureno.

"Manchester City inanunua mabeki wa kushoto na kulia kwa gharama za washambuliaji", aliongeza.

Mourinho ambaye aliteuliwa kuwa mkufunzi wa United mnamo mwezi Mei 2016 na kuvunja rekodi ya dunia alipomnunua kiungo wa kati Paul Pogba kwa kitita cha £89m, Eric Bailly kwa kitita cha £30m na kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kwa £26. 3m.

Mwaka huu alimnunua Romelu Lukaku kwa £75m, beki Victor Lindelof kwa £31m na Nemanja Matic kwa £41m.
 
Anachokiongea mou ni sawa kabisa, bodi ya Manchester ni ya kik*ma sana
 
Huo mpunga tukipewa sisi Arsenal tunatwaa mpaka kombe la dunia hakyababa
Katika mashabiki wenye mioyo ya uvumilivu ni wa Arsenal. Huyo Kocha kawapatia kweli kama alienda kwa mganga
 
Perisic a likuwa anauzwa 50 pound,alikataa kutoka hela ilihali United board walikuwa tayari kutoka hela
Aache guardiola anatengeneza Timu ya miaka 3 Mbele mournihno yeye anatengeneza ya kesho
Soka limebadilika Staili ya kupak bas iliishapitwa na Wakat
 
Njoo mumuone mwingine huyu! Aliyekataa kuongeza hela ya perisic ni mourinho?

Kama hujui bora ukae kimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…