Jose Mourinho akilalamikia kiwango cha fedha cha £300m alichopewa kununua wachezaji kuwa hakitoshi

Uwezo wake umeisha hapo, asituletee upuuzi, hela yote hiyo? Kama vipi ajiuzulu tu
 
Morinyo na Polepole walisoma chekechea moja ya kujifunza kutoa visingizio sema polepole alifeli morinyo akaingia darasa la kwanza
Huu mfano sio wa nchii hii[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa dau la £300m alilotumia kuimarisha kikosi chake hazitoshi.

''Tuko katika mwaka wa pili kujaribu kujenga timu ambayo unajua sio miongoni mwa timu bora duniani'', alisema raia huyo wa Ureno.

''Manchester City inanunua mabeki wa kushoto na kulia kwa gharama ya washambuliaji,” aliongezea.


Mourinho ambaye aliteuliwa kuwa mkufunzi wa United mnamo mwezi Mei 2016 na kuvunja rekodi ya dunia alipomnunua kiungo wa kati Paul Pogba kwa kitita cha £89m, Eric Bailly kwa kitita cha £30m na kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kwa £26.3m.

Mwaka huu alimnunua Romelu Lukaku kwa £75m ,beki Victor Lindelof kwa £31m na Nemanja Matic kwa £41m.
 
TETESI ZA USAJILI DIRISHA LA JANUARY.... ALHAMISI 28/12/2017.

1.KLABU ya Liverpool Imefanikiwa kumsajili rasmi Beki wa Southampton Mdachi, Virgil Van Dijik kwa ada ya uhamisho wa pauni £75m huku atakuwa akipokea Mshahara wa pauni £180,000 kwa wiki.Imeelezwa kuwa nyota huyo atakabidhiwa jezi no.4 na atatua Anfield Jumatatu ijayo ya tarehe 1.

2.MANCHESTER UNITED imejitoa kwenye mbio za kutaka kumsajili Winga wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann hivyo kuipa nafasi kubwa Fc Barcelona kumsajili Mfaransa huyo kwa pauni £89m.

3.CRYSTAL PALACE & BURNLEY & EVERTON zinapigana vikumbo kuiwania saini ya Mshambuliaji wa Angers ya Ufaransa, Karl Toko Ekambi.Fowadi huyo wa Cameroon amefunga mabao 9 katika Ligue 1 msimu huu.

4.WATFORD itampa mkataba wa miaka mitano Mshambuliaji wake , Abdoulaye Doucoure ambaye anatakiwa na Arsenal.

5.WINGA wa Borussia Dortmund Andre Schurrle anakaribia kujiunga na Stuttgart kwa mkopo.

6.PSG wanamtaka Kiungo wa Manchester United Marouane Fellain kwa uhamisho huru.Mbelgiji huyo atakuwa huru Jumatatu ya tarehe 1 kujiunga na klabu yoyote japo Galatasaray wanahitaji huduma yake.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…