Jose Mourinho ataweza kuuvunja mfumo usio wa soka, unaoongoza soko Uturuki?

Jose Mourinho ataweza kuuvunja mfumo usio wa soka, unaoongoza soko Uturuki?

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
José Mourinho: "Nataka kusafisha mpira wa miguu wa Uturuki, nataka kuvunja utawala wa Galatasaray, lakini huu ni utawala wa mfumo. Na hii ndio inafanya kazi kuwa ngumu. Kwa hiyo, nafanya kazi kwa bidii na Fenerbahçe ili kuvunja mfumo huu wa utawala.

Siku moja nilifungiwa mechi 4, picha za mkuu wa bodi ya nidhamu ziliibuka zikimuonyesha anashangilia akiwa amevaa jezi ya Galatasaray. Hii ndio njia pekee yakuelewa zaidi tukio hili."

●José Mourinho juu ya madai ya ubaguzi ya Galatasaray: "walikuwa hawana busara kunishambulia mimi kwa sababu hawajui utangulizi wangu, uhusiano wangu na Africa, watu wa Africa, wachezaji wa Africa, misaada ya Africa. Kwa hiyo, baada ya hili kuwa dhidi yangu, nadhani limewarudia wenyewe Galatasaray."
FB_IMG_17418080828280373.jpg

Via: Sky Sports
 
Kwani jamaa nini kilitokea?
Kwenye mchezo wa derby kati ya Galatasaray na Fernebance.... Mourinho alisema waliokuwa kwenye benchi la Galatasaray walikuwa wanaruka ruka kama nyani

Waturuki wakausisha kama ni kejeli kwa waafrica wanaonekana kama nyani mbele ya watu weupe ilhali Mourinho akumaanisha hivyo

Baada ya hapo wakampiga ban ila wachezaji wengi wa Africa walimtetea akiwemo Drogba
 
Back
Top Bottom