Uchaguzi 2020 Joseph Mbilinyi (Sugu): CHADEMA ikichaguliwa kuongoza sadaka zitaongezeka kwenye nyumba za ibada

Uchaguzi 2020 Joseph Mbilinyi (Sugu): CHADEMA ikichaguliwa kuongoza sadaka zitaongezeka kwenye nyumba za ibada

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ameomba viongozi wa dini wawaombe waumini wawachague wagombea kutoka chama hicho ili wananchi waweze kutoa sadaka kwenye nyumba za ibada.

Sugu aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni kwenye kata ya Maendeleo. Alisema maisha ni magumu na sadaka zimepungua makanisani kwa kuwa waumini hawana fedha hivyo kusababisha viongozi wa dini nao kuishi maisha magumu.

“Viongozi wa dini niwaombe sana… Sio tu mtuombee kwa Mungu ili tushinde Oktoba 28...bali pia mtuombee kura kwa waumini wenu kwa sababu serikali ya Chadema ina sera nzuri za uchumi zinazokwenda kurudisha kipato kwenye mifuko ya waumini wenu ili sadaka ziongezeke…ili fungu la kumi liongezeke… ili zaka ziongezeke na kazi ya Mungu iendelee...kwa sababu sisi Mbeya ni wacha Mungu ndugu zangu,” alisema Mbilinyi.

Aliomba wananchi waliojiandikisha kupiga kura wasikubali kurubuniwa na watu wanaopita majumbani kuulizia vitambulisho
 
Ni Mgombea Ubunge kupitia CHADEMA Jimbo la Mbeya Mjini amewaomba viongozi wa dini kuwahimiza waumini wao kuichagua CHADEMA katika uchaguzi wa ujao, kwani CHADEMA ikishika nchi na sadaka zitaongezeka kwenye nyumba za ibada!
Hii imeandikwa ukurasa wa ngapi kwenye ilani ya chadema? Au kuishiwa hoja na kubweka tu!
 
CHADEMA WAKICHAGULIWA SADAKA ZITAONGEZEKA-SUGU

MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ameomba viongozi wa dini wawaombe waumini wawachague wagombea kutoka chama hicho ili wananchi waweze kutoa sadaka kwenye nyumba za ibada.

Sugu aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni kwenye kata ya Maendeleo. Alisema maisha ni magumu na sadaka zimepungua makanisani kwa kuwa waumini hawana fedha hivyo kusababisha viongozi wa dini nao kuishi maisha magumu.

“Viongozi wa dini niwaombe sana. Sio tu mtuombee kwa Mungu ili tushinde Oktoba 28, bali pia mtuombee kura kwa waumini wenu kwa sababu serikali ya Chadema ina sera nzuri za uchumi zinazokwenda kurudisha kipato kwenye mifuko ya waumini wenu ili sadaka ziongezeke, ili fungu la kumi liongezeke, ili zaka ziongezeke na kazi ya Mungu iendelee, kwa sababu sisi Mbeya ni wacha Mungu ndugu zangu,” alisema Mbilinyi.

Aliomba wananchi waliojiandikisha kupiga kura wasikubali kurubuniwa na watu wanaopita majumbani kuulizia vitambulisho
 
Maajabu kuna mtu anaona sifa sadaka kupungua kwenye nyumba za ibada. Gharama za maisha zinaongezeka mishahara haijapanda miaka mitano, halafu anajiita Rais wa wanyonge.
 
Wao Chadema ndio tatizo kubwa LA sadaka kukosekana makanisani sababu wanakusanya sadaka kwenye mikutano yao ikiwemo ya Tundu Lisu kiasi kuwa waumini wakienda kanisani jumapili wanakuwa hawana hela za sadaka hela zote za sadaka anakuwa kachukua Lisu na wagombea wake kwenye mikutano yao kampeni

Kwa hiyo wanalazimisha kuchaguliwa kuwa mkituchagua ndipo tutawaambia wafuasi wetu acheni kutoa mikutano yetu toeni kanisani
 
Back
Top Bottom