Joseph Selasini achaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti NCCR Mageuzi

Joseph Selasini achaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti NCCR Mageuzi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mkutano Mkuu wa dharura wa chama cha NCCR-Mageuzi umemchagua Joseph Selasini kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho.

Selasini amechaguliwa katika uchaguzi uliofanyika leo Jumamosi Septemba 24,2022 katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma.

Katika uchaguzi huo, Selasini amepata kura 173 kati ya 232 zilizopigwa katika uchaguzi huo, huku mshindani wake Jerehemiah Maganga akipata kura 59.

Akizungumza mara baada ya kuchakuguliwa kushika nafasi hiyo, Selasini amesema katika uongozi wake atatekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi zote.

“Aliyekuwa makamu mwenyekiti alikitumia kifungu cha Katiba cha kuwa msemaji wa chama kuwafunga midomo viongozi wote, sasa unaweza kukisema chama katika eneo lako,” amesema.

Naye Maganga ameshukuru wajumbe kwa uamuzi waliofikia na kusisitiza kuwa huo ni uamuzi na kusisitiza haja ya viongozi walichanguliwa kuhakikisha wanawaunganisha wanachama wote kuwa kitu kimoja.

MWANANCHI
 
Hiyo NCCR imeshapoteza ushawishi wake, imekuwa kama CUF chini ya Lipumba. Hivyo vitakuwa ni vyama vitakavyotuniwa na ccm ili iendelee kukaa madarakani kwa shuruti.
 
Kukimbia CHADEMA ilikuwa ni kuwahi kuizika NCCR.
 
Hiyo NCCR imeshapoteza ushawishi wake, imekuwa kama CUF chini ya Lipumba. Hivyo vitakuwa ni vyama vitakavyotuniwa na ccm ili iendelee kukaa madarakani kwa shuruti.
Mbona Chadema hujakitaja hapo. Unafikiri kina tofauti na NCCR-MAGEUZI na CUF?
 
Wamemchagua DEFAO toka Rombo))
Wamebugi sana ukishaona mtu mzima anapaka mavitu kichwani ujue kichwa kina shida kubwa katika utendaji wake.))
 
Back
Top Bottom