Josephat Gwajima akana utajiri wake

Kwa sasa Gwajima amekuwa ni kama mtu aliyerukwa na akili....hana tena uwezo wa kupima matamshi yake....ni sawa na mtoto mdogo anayejifunza kuongea....bado nazitafakali akili za hao anaowaongoza kuwa zipo chini kwa kiwango gani.......maana kwa mtu mwenye ufahamu ni aibu kuwa na kiongozi wa kiroho wa aina hiyo....kiongozi wa kiroho asiyeweza hata kumiliki ulimi wake mwenyewe anawezaje kuwachunga kondoo wa bwana na kuwafikisha nchi ya ahadi??.....kiongozi wa kiroho anayehubiri utengano na sio mshikamano ni sumu katika nchi hii inayojitangaza kwa amani na utulivu.....ni mwehu pekee ndiye ambaye anaweza kuwa mfuasi wake kwa kuwa hata kwenye msafara wa mamba pia kenge hawakosekani.....kitendo cha kumwambia mheshimiwa raisi kuwa awaambie hao polisi kuwa wasimfuatilie fuatilie kwa maana kuwa mambo yake hayawahusu kinaoyesha ni jinsi gani huyo kiongozi wa kiroho asivyo na heshima hata kwa mamlaka za dunia kama walivyoa mrishwa na huyo wanayemtumikia....jeshi la polisi kama lina mashaka na vyanzo vyake vya fedha kwanini asihojiwe...kwani yeye yupo juu ya sheria...???....bado waumini wake wanamshangilia na kummiminia fedha kwenye makapu......KWELI DUNIA MSONGAMANO........
 

Dah! Rais wetu naye sijui atamkemea!(atamtukana)
 
Mwenzako anakwambia ana waumini 70000 kila mtu akimpa 10000 ana mil.700 ndani ya nusu saa tu.upo ndugu?
sasa wewe na yeye nani ana porojo
Hesabu inakataa,kwanza waumini wote hawawezi kuwa na hiyo 1000,achilia mbali 10,000.
pia hawawezi wote kutoa.
hata calculation za mda zinakataa.
hata kama itachukua sekunde moja kwa mtu kuitumia kutoa,ina maana ili wote elfu 70,wafanye tu kufikiwa na kutoa watachukua hata siku mbili.ukichukulia siku moja ina dakika hazifiki hata mia nane.utaratibu wa kila muumini kutembea hadi mbele na kutoa ,hadi waumini wote elfu 70 waishe ni mda mrefu sana.
 
Kwa maneno aliyoongea angekuwa kiongozi wa dini wa upande mwengine angeambiwa hana elimu.
 
Huyu jamaa sasa ukichaa unampanda.
Kawaida kanisa linakuwa na kumbukumbu za waumini wake pamoja na collections za kila ibada.
Anafanya ibada za kihuni huni halafu sasa analeta stori za vijiweni.
Inabidi aonyeshe hao waumini 70,000 waliko na kumbukumbuza michango yao.

Thadhari kwa wale walio karibu naye , asifikiri anaongea na mbumbumbu, lazima kuna kitu nyuma ya pazia.
 

Mkuu hajui kuna wataalamu wa hesabu za QUEING wenyewe wanaita queing theory Ambapo unaweza compute misururu iwe ya kutoa sadaka au vyovyote ukajua idadi ya waumini kwa dakika tu bila hata kuambiwa.

Uwanja wa Tanganyika packers anaposalia Gwajima unaweza chukua watu elfu tatu tu maximum kutokana na ukubwa wake.Tena hao watu wawe wamesimama sio wamekaa.Hao wa kusema elfu sabini ni porojo tena porojo za uwongo hasa.Porojo hizo huwa wanazitumia kudanganyana kuonyeshana nani ana watu wengi!!
 
Sasa nimeanza kupata picha huenda huyu bwana mdogo alitumiwa kummaliza mchungaji, na lile lilikuwa jaribu la kwanza na lilishindwa. Hili ni jaribu la pili lakini kwa upande mmoja mjaribiwa kaliruhusu mwenyewe, na wajaribu wakapatia nafasi.

Mkuu,sisi hapa tunaspeculate mambo tu, ukweli anaujua Mungu.
 
Tanzania inaitaji watu majasiri kama mchingaji Gwajima,
Nampenda sana huyu mch kwasababu uhwa hapindishi maneno kama watu wengine,

Ni bora kuwa kama Mch Gwajima,ambaye anasimamia kweli hata kufa.
 
Sijui anadhani anamdanganya nani,wakati watu wanaweza calculate ukubwa wa kiwanja na mita kadhaa na wakajua capacity yake ya kubeba watu.
 

Hivi ni lazima kutetemeka wakati unaandika mada yako??? Nia yako ni Ubishi au ni kusisitiza nini?? Maana inakuwa kama unataka kununua ugomvi wa Gwajima na Polisi?? Na unavyojibu ni kama wewe ndio polisi au serikali??
 
Watu 70,000 NI zaidi ya watazamaji watakaopata kuangalia mechi uwanja wa Taifa(mechi ya Stars na The Mamba).
Hizo sadaka NI za kanisa au za kwake Gwajima?
Kanisa NI Taasisi. Iweje iwe Mali ya MTU mmoja?
Makanisa haya ya akina Getrude NI hatareee.
 
Tanzania National Main Stadium is a multi-purpose stadium in Dar es Salaam, Tanzania. It opened in 2007 and was built adjacent to Uhuru Stadium, the former national stadium. It hosts major football matches such as the Tanzanian Premier League and home matches of the Tanzania national football team.
With 60,000 seats it is the eleventh largest stadium in Africa and the largest stadium in Tanzania.
It is owned by the Tanzanian Government. The stadium was built by Beijing Construction Engineering Group at a cost of $56 million.
Source: Wikipedia

My Take
Itabidi "askofu" Gwajima atueleze hao waumini waliwaweka wapi pale Tanganyika Packers ilhali hakuna nafasi ya kuwaweka hata watu 5,000.
Njia ya mtu mwizi, mwongo na laghai ni fupi.
Sasa anavunja amri ya saba kushuhudia uongo.
 

Mkuu unaijua complimentarity principle? Kifupi ni hivi, watu wawili tu wakitoa elfu tano tano wamewabeba watu nane ambao hawajatoa senti moja. Kwa hiyo kama ilivyo ngumu kwa wote kutoa buku buku ndio hivyo hivyo ngumu kukosa watu watao toa zaidi ya buku. Katika swala la mda unapungua kutegemea na idadi za boxes za kutumbukizia sadaka.
 
Kitaalamu,mtu mmoja akiwa wima,anachukua sguare feet 2.
sasa kwa watu elfu 70,ina maana tanganyika packers ina ukubwa wa sguarefeet 140,000?
watalamu mnaweza calculate tujue ni mita ngapi ama kilomita ngapi hizo.
 
Ningekua hapo bongo ningeifanya hii personal project kwa kuhudhuria pale ili kuanalyse ni kweli hii mambo ama ni magumashi.
umetoa reasoning ambayo inafikirisha japo capacity ya uwanja bado haikubaliani.
halafu kama watapatikana sema watu 2000,wakatoa elfu kumikumi.
na watu 3000 wakatoa elfu tanotano.
bado hesabu inakataa kufikisha hiyo milioni 70 achilimbali milioni 700.

hapa wakuu ametudanganya.
 
Kitaalamu,mtu mmoja akiwa wima,anachukua sguare feet 2.
sasa kwa watu elfu 70,ina maana tanganyika packers ina ukubwa wa sguarefeet 140,000?
watalamu mnaweza calculate tujue ni mita ngapi ama kilomita ngapi hizo.

Mkuu hizo squarefeet 140000 za kutosha watu elfu 70 ni sawa na ekari 32.Sasa pale Tanganyika packers pana ekari 32? Gwajima mwongo mkubwa.Pale anapotumia hata hekari tatu hazifiki.

Uwanja wa taifa unaweza himili hiyo idadi ya elfu sitini kwa kuwa umejengwa kwa mfumo wa ghorofa (ngazi ngazi) lakini ungekuwa flat wasingetosha.Gwajima kwa hili la Elfu 70 watu kuhudhuria pale ni uongo tena wa mchana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…