KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Unavyokula sio kweli ni vyakooo!!!!! Na hapo unaposhupaa ndipo unapoonyesha kwamba umejaa ukungu kwenye ubongo wako wa nyuma!
Kwa jinsi ulivyo panic bila shaka wewe ni miongoni mwa misukule unayomtajirisha GWAJIMA...
I cant reduce myself into your level of thinking! Wewe endelea na mapambano yako na Gwajima wenu, Zitto kabwe, na mkienda sana chadema na ACT. Narudia, kama baba yako hakukukufundisha kufikiri na ukaishia hapo, I am not responsible for your zombie like attitudes!
Kumropokea maneno ya kashfa mtu anayelingana na baba yako ni kumwambia ukweli au kumtukana....au wewe baba yako akikukosea au mkipishana kauli ndio unatumia lugha aliyoitumia gwajima kumweka sawa baba yako....??
Walokole wakiwa katika tabu, ndiyo kwanza wanashikamana,ukitaka kuwasambaratisha wape neema utafanikiwa. Wakipata nyumba nzuri, gari zuri, kazi nzuri na safari katika nchi mbalimbali wanaacha kuja kanisani lakini wakiwa katika matatizo wanashikamana, hamuwezi kuwasambaratisha, alisema.
meet them at the great pond.
Sijui anadhani anamdanganya nani,wakati watu wanaweza calculate ukubwa wa kiwanja na mita kadhaa na wakajua capacity yake ya kubeba watu.
hapa ndipo Gwajima alipokosea lakini yalishaisha baada ya Pengo kumsamehe .
Huyu jamaa sasa ukichaa unampanda.
Kawaida kanisa linakuwa na kumbukumbu za waumini wake pamoja na collections za kila ibada.
Anafanya ibada za kihuni huni halafu sasa analeta stori za vijiweni.
Inabidi aonyeshe hao waumini 70,000 waliko na kumbukumbuza michango yao.
Thadhari kwa wale walio karibu naye , asifikiri anaongea na mbumbumbu, lazima kuna kitu nyuma ya pazia.
Mkuu hizo squarefeet 140000 za kutosha watu elfu 70 ni sawa na ekari 32.Sasa pale Tanganyika packers pana ekari 32? Gwajima mwongo mkubwa.Pale anapotumia hata hekari tatu hazifiki.
Uwanja wa taifa unaweza himili hiyo idadi ya elfu sitini kwa kuwa umejengwa kwa mfumo wa ghorofa (ngazi ngazi) lakini ungekuwa flat wasingetosha.Gwajima kwa hili la Elfu 70 watu kuhudhuria pale ni uongo tena wa mchana.
Kwa sasa Gwajima amekuwa ni kama mtu aliyerukwa na akili....hana tena uwezo wa kupima matamshi yake....ni sawa na mtoto mdogo anayejifunza kuongea....bado nazitafakali akili za hao anaowaongoza kuwa zipo chini kwa kiwango gani.......maana kwa mtu mwenye ufahamu ni aibu kuwa na kiongozi wa kiroho wa aina hiyo....kiongozi wa kiroho asiyeweza hata kumiliki ulimi wake mwenyewe anawezaje kuwachunga kondoo wa bwana na kuwafikisha nchi ya ahadi??.....kiongozi wa kiroho anayehubiri utengano na sio mshikamano ni sumu katika nchi hii inayojitangaza kwa amani na utulivu.....ni mwehu pekee ndiye ambaye anaweza kuwa mfuasi wake kwa kuwa hata kwenye msafara wa mamba pia kenge hawakosekani.....kitendo cha kumwambia mheshimiwa raisi kuwa awaambie hao polisi kuwa wasimfuatilie fuatilie kwa maana kuwa mambo yake hayawahusu kinaoyesha ni jinsi gani huyo kiongozi wa kiroho asivyo na heshima hata kwa mamlaka za dunia kama walivyoa mrishwa na huyo wanayemtumikia....jeshi la polisi kama lina mashaka na vyanzo vyake vya fedha kwanini asihojiwe...kwani yeye yupo juu ya sheria...???....bado waumini wake wanamshangilia na kummiminia fedha kwenye makapu......KWELI DUNIA MSONGAMANO........
Mkuu mimi kama mkristo nachukia sana wizi, uongo na ulagghai, kama wa self made "askofu" Gwajima.Sakata la GWAJIMA NI SHAMBULIO KWA ukristo mbona hatuoni haya kwenye MISIKITI yenu?????
ASKOFU Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, amesema yeye si tajiri kama inavyodhaniwa, bali alichonacho ikiwa ni pamoja na nyumba, magari na helikopta ni baraka tu za Mungu, lakini kama ni utajiri, anatarajia siku moja utamshukia.
Aliyasema hayo jana wakati akihubiri kanisani kwake Kawe, Dar es Salaam, ambako alisema anawashangaa watu wanaomfuatilia maisha yake huku wakisema yeye ni tajiri mkubwa.
Wanaodai mimi ni tajiri wana wivu tu na wananionea, mimi si tajiri, bali ni masikini kama walivyo masikini wengine. Natarajia kutajirika hapo baadaye waumini wangu wakiwa matajiri, siwezi kutajirika kama waumini wangu bado ni masikini, nitatajirika pamoja nao, alisema Gwajima.
Kuhusu mgogoro unaoendelea baina yake na Jeshi la Polisi, Askofu Gwajima alisema yeye anauona kama ni vita vya kiroho na hivyo ataendelea kumwomba Mungu ili amsaidie kupambana na kilichopo mbele yake na anaamini kuwa atashinda vita hiyo kwa uweza wa Mungu anayemtegemea.
Mungu wangu na awasamehe wote wanaonituhumu kuwa mimi ni tajiri na kuamua kudhoofisha huduma, nasema huduma yangu haitakufa kamwe na wala hatutayumba katika mipango yetu ya kuhubiri injili. Tutapigana kwa uweza wa Mungu na tutashinda kama alivyosema kuwa tutapigana pamoja naye na tutashinda, alisema Gwajima.
Akizungumzia afya yake, Askofu Gwajima alisema kwa sasa anaendelea vizuri na anaweza kusimama na kutembea, kuhubiri kama ilivyokuwa hapo awali na hatarajii kurejea tena kwenye kiti cha baiskeli ya magurudumu matatu bali atasimama imara daima.
Kuhusu kupeleka nyaraka kadhaa anazotakiwa aziwasilishe polisi siku ya mahojiano Aprili 16, mwaka huu, Askofu Gwajima alisema suala hilo bado wanasheria wake wanalishughulikia na wataendelea kufuata taratibu zote zinazotakiwa na jeshi hilo.
Gwajima anatakiwa kuwasilisha nyaraka muhimu za hati ya usajili wa kanisa lake, namba ya usajili wa kanisa, hati ya umiliki wa helikopta, hati ya nyumba anazomiliki, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake pamoja na hesabu za fedha za kanisani kwake zinazohusu mapato na matumizi.
Nyaraka zingine ni majina ya Bodi ya Udhamini wa kanisa, mpiga picha za video kanisani kwake siku ya ibada na shughuli zingine za kanisani hapo pamoja na waraka wa Maaskofu uliosomwa makanisani ambao Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alioupinga na kusababisha yeye kumkashifu kiongozi mwenzake huyo wa dini.
Akionekana kuwa makini sana na lugha anayotumia wakati wa kuhubiri, Gwajima aliwaomba waumini wake waendelee kufuatilia kila sehemu na kuchunguza mambo yote mabaya yanayosemwa juu yake na kanisa lake na kuyaripoti kwake au kwa uongozi wa kanisa ili wayafanyie kazi mara moja kabla hayajaleta madhara.
Nawaombeni sana mfuatilie kila chanzo cha habari na kuchunguza mambo yote yanayosemwa juu yangu au kuhusu kanisa na kuyaleta mara moja hapa kanisani ili tuyafanyie kazi kabla hayajaleta madhara makubwa, alisema Gwajima.
Aliongeza kuwa, tuendelee kuwa na umoja katika kipindi hiki ambapo shetani anataka kupigana nasi ili tuweze kushinda. Tukifarakana hatutaweza bali tukiwa kitu kimoja tutasonga mbele na kuwa huru.
Utajiri wake
Wakati akikana kuwa tajiri, mwanzoni mwa mwaka jana alifanya mahojiano na gazeti hili na kukiri Mungu anambariki, ndiyo maana mambo yake yanamnyookea.
Aliyasema hayo alipokuwa anazungumzia mpango wake wa kununua helikopta kwa ajili ya huduma za injili ndani na nje ya nchi.
Alikiri kutokana na utajiri anaosema unatokana na baraka za Mungu, anamiliki jumba la ghorofa nne eneo la Mbezi Beach katika Manispaa ya Kinondoni.
Pia amewanunulia wachungaji wake 40 magari ya kutembelea kwa bei tofauti, yakiwemo ya chini ya Sh milioni 10 na mengine ya zaidi ya Sh milioni 20.
Ni kweli nimewanunulia magari, unajua moja ya misingi yangu ya maisha ni kwamba, mimi siwezi kuishi maisha mazuri, wakati wachungaji wangu wanadhalilika, nimewanunulia magari karibia 40. Lakini nina wachungaji wa ngazi mbalimbali, hawa ni wale wa juu, wengine wachungaji wadogo wapo zaidi ya 670, hawa ni watenda kazi muhimu na wanatofautiana kwa ngazi zao, ndio maana kazi ya Mungu inasonga mbele hata nisipokuwepo, alisema Gwajima.
CHANZO: Habari Leo
duh. haya masikini ana 'hedikopta' na jumba la ghorofa nne! nchi hii hii
Pole ndugu yangu na kitochi chakoMi sipendi mtu anaye qoute habari ndeefu kama hii alafu anaandika uharoo, wengine tunatumia vitochi bana haaa
Mimi sipo patakapozuka TIFU na walokole wake maana wanasubiri DNA tu
- linganisha pua ya mtoto na baba yake halisi utampata tu
- linganisha paji la uso