Joshua alilisimamisha Jua

Jiulize wewe, jua, Joshua mmetokana na nini? Iko nguvu kubwa izidiyo upeo wa mwanadamu kufikiria. Hiyo nguvu ndiyo Mungu muweza, muumba na mmiliki wa vyote
Kama hiyo nguvu ni kubwa imezidi upeo wa mwanadamu mbona kuna watu (wachungaji, mashekh, mapadri n.k) wanadai wanaupeo kuhusu mungu na huwa wanatueleza mengi kuhusu yeye? Tena huwa wanatumia vitabu ambavyo kimsingi vimeandikwa na mwanadamu.
 
Poles mkuu na wewe umepitiwa na propaganda za flat earth society?????
 
Acha kuharibu thread za watu
Ungeanzisha yako!
Also up Uzi wa hiyo propaganda
Pia kumbuka!! Dunia SIYO FLAT!!!!!
 
Kosa lako ni hapo uliposema jua halizunguki kwenda kokote.Ni kweli dunia huzunguka,lakini pia kuanzia leo tambua jua nalo huzunguka tena kwa spidi kali sana ya Kilomita 828,000 kwa saa. Na hutumia miaka Milioni 230 kukamilisha mzunguko mmoja pamoja na hiyo spidi kali.

Kwa Joshua,nadhani alikuwa duniani wakati analisimamisha jua.
Asante!!
 
Kama hiyo nguvu ni kubwa imezidi upeo wa mwanadamu mbona kuna watu (wachungaji, mashekh, mapadri n.k) wanadai wanaupeo kuhusu mungu na huwa wanatueleza mengi kuhusu yeye? Tena huwa wanatumia vitabu ambavyo kimsingi vimeandikwa na mwanadamu.

Hao wanadamu wametumiwa na Mungu/Hiyo nguvu kuu ipitayo upeo wa mwanadamu.
 
Na sijui nani alidhibitisha kwamba jua kweli lilisimama....hv vitabu wakati mwingine inabidi tuviangalie kwa jicho la tatu, maana pekua pekua yangu kwenye hv vitabu sijaona hata sehemu moja ya aya kuna [HASHTAG]#saini[/HASHTAG] ya mungu kudhibitisha alichokiongea kweli ni yeye au ujanja tu wakibinadamu waweze kutawala kiurahisi au ajira za watu....
 
Joshua alipojua wenzake wanatumia nguvu za kutoka kwenye jua vitani, alilisimamisha na ndio maana alipata ushindi. Ulimwengu wa roho una mambo mengi sana
 
Acha stori mkuu, hizo ni hadith za BETINA
 
Jiulize tena alitumia uwezo gani kulisimamisha jua
 
sasa hapo alisimamisha jua ama dunia? maana tunajua kuwa dunia ndo inayozunguka
 
Ile verse inasema Ivii "Then Joshua spoke to the Lord on the day when the Lord delivered the Amorites before the children of Israel; and he said in the sight of Israel: ‘Sun, stand still [dom] upon Gibeon; and you, Moon, in the valley of Ayalon.'” (Joshua 10:12). Tunaona wanaongelea na Mwezi hapo so possibly speaking this would have been a SOLAR ECLIPSE happening ndo maana akatumia neno DOM ambalo lmetumika kwenye (Psalms 37:17) meaning standing still huku mwezi ukipita katkat ya Jua na Dunia!
 
sasa hapo alisimamisha jua ama dunia? maana tunajua kuwa dunia ndo inayozunguka
Huna uwezo wakujua kuwa dunia inazunguka zaidi ya kuambiwa ila uwezo wa kujua Jua linazunguka upo Machoni mwako siku zote ila haukuambiwa hivyo!
 
Huna uwezo wakujua kuwa dunia inazunguka zaidi ya kuambiwa ila uwezo wa kujua Jua linazunguka upo Machoni mwako siku zote ila haukuambiwa hivyo!
we huamini uwepo wa Mungu kwakuwa huna uwezo wa kumuona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…