Uchaguzi 2020 Joshua Lawrence kutoka mkoani Mbeya, amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Joshua Lawrence kutoka mkoani Mbeya, amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
1594394910069.png
Joshua Lawrence kutoka mkoani Mbeya, amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais kupitia chama cha ACTwazalendo.

Kasema endapo atapewa ridhaa ya kuongoza nchi, atashughulikia mambo 2 ikiwemo kilimo na ufugaji kwa kuhakikisha kila mwananchi anafuga kuku wasiopungua 1000.

===

Joshua Lawrence kutoka Mkoani Mbeya amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania Urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo na kuahidi kuhakikisha kila mwananchi atafuga Kuku wasiopungua 1000.

Ametaja vipaombele vyake kuwa,ni kuwekeza katika kilimo cha mazao ya chakula na biashara, elimu ya ufugaji kuku, na kuhakikisha elimu ya bangi katika kuzalisha nyuzi za viwanda na chakula cha kurutubisha mifugo kama kuku.

“Nikizungumzia bangi si wawe wanavuta, bali ni kuwawezesha kujua madhara yake na faida wenzetu wanayoipata katika mataifa makubwa yenye virutubisho katika ulishaji wa chakula cha kuku na kuzalisha nyuzi za kutengenezea nguo kama ilivyo kwa zao la pamba” Amesema mgombea huyo.

Katibu wa ACT – Wazalendo mkoa wa Mbeya, Geofrey Sanga amesema tangu kuanza uchukuaji fomu, wamepata wagombea ubunge majimbo ya Mbeya, Rungwe, Mbarali na mmoja wa Urais.

Ikumbukwe kuwa hii itakuwa mara ya pili kwa ACT – Wazalendo kusimamisha mgombea Urais baada ya Anna Mghwira kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa mwaka 2015.
 
Joshua Lawrence kutoka mkoani Mbeya, amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais kupitia chama cha ACTwazalendo.

Kasema endapo atapewa ridhaa ya kuongoza nchi, atashughulikia mambo 2 ikiwemo kilimo na ufugaji kwa kuhakikisha kila mwananchi anafuga kuku wasiopungua 1000.
Atafuta kuonekana apate uteuzi tu, mbona hatumfahamu?
 
Back
Top Bottom