Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Nimeona Nyaraka kutoka Mahakama ya Rufani Tanzania kuwa shauri la Madai Nambari 342 la mwaka 2019 kati ya Joshua Samwel Nassari dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muunganon wa Tanzania limepangwa kusikilizwa mnamo tarehe 30 mwezi Septemba kwama huu. Shauri hilo lililopo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania lipo mbele ya Majaji wa Rufaa watatu (Mhe. Mkuye, Mhe. Wambali na Mhe. Korosso).
Kwa kutazama kilichojiri hadi sasa tangu Nassari apoteze Ubunge wake wa Arumeru Mashariki (mfano Bunge kumaliza muda wake; Nassari kuhamia CCM na Nassari kugombea tiketi ya CCM Arumeru Mashariki kabla ya Wajumbe kufanya yao), kuna uwezekano wowote wa Nassari kuendelea na shauri lake dhidi ya Spika wa Bunge?