Joslini kapotekea wapi wadau!"!

mbwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2018
Posts
1,174
Reaction score
2,912
Niende moja kwa moja kwa huyu mwamba joslini mzeee Wa pafyumu yaani alitikisa balaaaa na baadhi ya nyimbo zake kama niite mpenzi,mshikaji mmoja,maisha yanatisha ft nuruel,huyu demu simwelew ft juma nature,nisikilize .Kiukweli huyu mwamba alikuwa yuko sawa kwenye gemu la bongo land ,mwenye kujua saiz amejikita na mishe gani na wapi alipo atujuze kidogo coz najua wengi wamemiss radha yake maana siku izi hamna mziki wenye radha kabisa zaidi ya kiki tu
 
Embu mtafute.....

Mshikaji mmoja hivi' ilikuwa kati ya pini kali sana.
 
Nadhani leo hii ukimuuliza mr blue wakati gani kwenye mziki ulikuwa mgumu kwake basi kama hatosema kipindi joseline anatoka atakuwa anaongopea


Joseline alikuja na style ya kuimba kama mr blue alafu akawa anatoa kitu baada ya kitu blue akadata

Dully akaona isiwe tatizo akawakalisha ndani ya ngoma moja, ebwana blue akampoteza vibaya joseline, baada ya hapo joseline akapotea vibaya blue tunaye mpaka leo

Nashangaa kwanini dully kashindwa wakalisha kiba na dai katika ngoma moja
 
Duuh Mkuu kwanza Karibu..Yani umejiunga tu na kuanzisha Uzi! πŸ˜€ ..au wewe ndiyo Joslini ? πŸ™‚ Kama Siyo fungua Kuna Uzi unawazungumzia Wasanii waliopotea Katika Muziki Kwa Bongo..Utapata Habari zake.
 
Nimeangalia kwenye yale majina
Ya wauza vidonge sijamuona

Sasa hata mchumba hajamtambulisha
 
Duuh Mkuu kwanza Karibu..Yani umejiunga tu na kuanzisha Uzi! πŸ˜€ ..au wewe ndiyo Joslini ? πŸ™‚ Kama Siyo fungua Kuna Uzi unawazungumzia Wasanii waliopotea Katika Muziki Kwa Bongo..Utapata Habari zake.
Hapana mkuu me ni nlikiwa invisible member Wa jf Sema sikutaka kujiunga mapema nikawa nafuatilia tu nyuzi za humu ila nipo hapa tokea 2012 nikiwa nasoma tu upepo Wa hapa jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…