Joti na Mpoki walivyomuigiza Jengua kafulia kwenye Orijino Komedi

Joti na Mpoki walivyomuigiza Jengua kafulia kwenye Orijino Komedi

Machudaa

Senior Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
123
Reaction score
311
Kile kipindi cha kipuzi Kwenye Orijino komedi TBC1 Umefulia kilidhalilisha wengi sana.

Mpoki alimuigiza Kama Jengua Muhammed FungaFunga eti kafulia. Huku Joti akimfuatafua na maswali kwanini kapotea.

Mpoki (Jengua) anamjibu mbona yupo tuu siku hizi vipindi vyake viko CNN na BBC. Joti akamjibu huku akijigaragaza chini mwongo wewee Umefulia.

Yani wale jamaa ni wapuuzi sana hata mmoja wao anayeumwa asionewe huruma.

Wameshawahi kuwaigiza na kuwadhalilisha.

Augustino Mrema
Edibily Lunyamila
Muumin Mwinjuma

Pia walimuigiza kwa kumdhalilisha Hasma Hamis Kidogo kafulia. Yule mwanamama mrembo aliyeimba taarab mapenzi ya dhati. Ilibidi irushwe hewani wiki iyo Wakaghairi kuirusha wiki iyo kwasababu aliaga dunia. Bila hata aibu Macregan ambaye alimuigiza akahudhuria msiba. Wapuuzi sana hawa majamaa.

Kipindi icho kilipigwa stop baada ya walipomuigiza Laurence Masha aliyejuwa Waziri wa mambo ya ndani wakati wa JK kwa kushindwa ubunge na kukosa kuteuliwa tena kwenye baraza la mawaziri. Sijui Macha alilalamika.

Walimdhalilisha pia mara kwa mara Lowassa na Mzee Mengi na John Komba.

Joti, Masanja, Mpoki, Wakuvanga na Vengu wameleta maumivu na udhalilishaji wa hali ya juu kwenye jamii. Ni wapuuzi.

R. I. P

Jengua
 
Bila ushahidi hata kidogo wa picha au kavidio itakuwa changamoto kukuelewa,japo nakumbuka ya Mrema tu aliigiza yule mgonjwa kwa kipindi fulani alikuwa anaugulia kwa kaka yake Kigamboni
 
Mie nakumbuka tu ya Komba walivyokua wakimuigiza dah Maisha haya!!!
 
Video haipo. Ni video moja tu ipo YouTube wakimdhalilisha kocha wa duniani Muumin Mwinjuma

Ila Joti alikua mpuuzi hatari, nilibahatika kukutana nae pale Ferry kwenye foleni alishuka kwa gari alikua nje anapunga upepo nikasema huyu dogo mbona kama namjua, kumuangalia fresh ndio nikagundua ni Joti. Yaani kalikua simpo bàlaa utadhani sio haka kanakofanya huu upuuzi!!
 
Walimdhalilisha pia marehemu Kanumba eti hajui kiingereza alipozuru nchi flani hivi. Vengu ndie alikuwa akimuigiza Kanumba.
 
Walimdhalilisha pia marehemu Kanumba eti hajui kiingereza alipozuru nchi flani hivi. Vengu ndie alikuwa akimuigiza Kanumba.
Ile kama kumbukumbu zangu ziko vizuri alikuwa kaenda kwenye mashindano ya Big brother Afrika kweli mjomba ngeli ilimshinda walimtoa mara moja.
 
Hakuna eliedhalilishwa
Comedy huwa anataniwa yoyote hata Malkia na Mfalme...

Mradi alietaniwa alikuwa hai hai ilikuwa haki yake kutaniwa..
Haimaanishi walitaka age au walifurahia kifo chake....tuache ushamba
 
Hakuna eliedhalilishwa
Comedy huwa anataniwa yoyote hata Malkia na Mfalme...

Mradi alietaniwa alikuwa hai hai ilikuwa haki yake kutaniwa..
Haimaanishi walitaka afe au walifurahia kifo chake....tuache ushamba
 
Back
Top Bottom