Joto la Uchaguzi lainyemelea pia Uganda, Waziri Mkuu apigwa 'Stop' kutafuta kuungwa mkono

Joto la Uchaguzi lainyemelea pia Uganda, Waziri Mkuu apigwa 'Stop' kutafuta kuungwa mkono

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Waziri Mkuu wa zamani wa Uganda ambaye pia aliwahi kushikilia wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha NRM Amama Mbabazi, anaendelea na ziara nchini Marekani na Barani Ulaya katika harakati zake za kutafuta uungwaji mkono azma yake kugombea urais mwakani.

Wakati huo huo huko Uganda, Mawakili wake wametoa msimamo wakipinga maagizo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Jenerali Kale Kayihura, kumtaka asitishe mara moja shughuli zake za kushauriana na wananchi mbalimbali kwa mujibu wa ratiba aliyowasilisha kwa Tume ya uchaguzi na kuruhusiwa kufanya hivyo.

11402894_1013787371999923_8133150104370879761_o.jpg


Chanzo: DW
 
Back
Top Bottom