Joyce Kiria na Wema Sepetu lindeni brand zenu

Joyce Kiria na Wema Sepetu lindeni brand zenu

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
joyce kiria.jpg

wema-sepetu-kali.jpg

Nimeangalia picha zinazozunguka mitandaoni za hawa mabinti mawili. Kwanza ya Joyce Kiria ambaye anadai mwanaume anayetaka kutoka naye hivi sasa ni lazima alipie gharama za vitu atakavyokuwa amevaa kwa asilimia sabini (70%).

Joyce inawezekana kabisa ana machungu toka kwenye ndoa yake ya kwanza ambayo imevunjika. Katikati ya maelezo yake inaonesha amepata "request' nyingi sana tangu ijulikane kwamba ameachana na mumewe.

Lakini kwenye maelezo yake inaonekana anakazia sana kurudishiwa gharama zake kuliko mahusiano na huyo mwenye kurudisha hizo gharama. Kiuhalisia ni kwamba yeyote mwenye kuweza kurudisha gharama kwa siku husika ndiyo atatoka naye.

Nimeona pia Video ya Wema Sepetu akiwa kwenye bwana la kuogelea. Kwanza jinsi anavyochezesha makalio yake na maneno anayoyasema na kijana aliye pembeni yake kwenye bwawa lile la kuogelea inatia kinyaa.

Nawaasa Wema na Joyce wajue kwamba maisha yao yanategemea sana ambayo wateja wao wakubwa ni wananchi wengi ambao hawapendi matendo na maneno ya kijinga.
 
unajuwa mtu akizeeka analudi utotoni ...sasa Joyce kilia sahv ameshagonga 50+ utamwabia nini shavu limeshadondoka....Alafu Wema Sepetu.... Njaa zinamcost na stress zakupata Mtoto...unajuwa Wema kinachomkost ni wanaume anaotoka nao ...yaani achezea zero distance... Mara yuko na Domo Mara yuko na Aslay...Mara yuko Chemical .
 
Kwa upumbavu huu wanaofanya,kuna Kampuni gani itawapa u Balozi kama wanavyolilia, wageni wataendelea kupeta
 
Nilidhani kwamba Joyce anaona Kampuni yake inayoendesha kipindi cha "mwanamke Live" na ile ya kufunza mayaya ni mambo ya muhimu kwenye maisha yake kuliko kunadi kutaka mwanaume atakayerudisha gharama ya nguo zake na mapambo (accessories) atakayokuwa amevaa siku ya kutoka matembezini.

Wema nadhani kuna wakati alikuwa anataka kuwa Mkurugenzi wa kampuni itakayokuwa inazalisha Filamu.
 
unajuwa mtu akizeeka analudi utotoni ...sasa Joyce kilia sahv ameshagonga 50+ utamwabia nini shavu limeshadondoka....Alafu Wema Sepetu.... Njaa zinamcost na stress zakupata Mtoto...unajuwa Wema kinachomkost ni wanaume anaotoka nao ...yaani achezea zero distance... Mara yuko na Domo Mara yuko na Aslay...Mara yuko Chemical .
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Back
Top Bottom