Joyce Kiria: Rais Magufuli anatukubali, tupambane

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Mwanaharakati wa haki za wanawake hapa nchini Joyce Kiria the Super woman kutoka Shirika la haki za wanawake Tanzania, amewataka wanawake wote nchini kuendelea kusimama imara katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi mwaka huu wa 2020.

Akizungumza na vyombo vya Habari mwanaharakati huyo amesema kwamba kwa muda wa miaka mitano ya Mh Rais Doctor John Pombe Magufuli kumekua na muamko mkubwa kwa wanawake kufanya kazi kwa bidii katika nafasi walizopewa bila kuwepo na utumbuaji

Kiria amewaomba wanawake kote nchini kujitokeze kufanya mabadiliko katika kugombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya udiwani ubunge kwa lengo la kushika nafasi na kusaidiana na Makamu wa Rais katika kupambania haki na uwajibikaji wa mwanamke .

"Namshukuru Mh Rais kwa kututhamini na kutupa nafasi katika uongozi wake kutupa nafasi akiwemo Mama Samia Suluhu ummy mwalimu mama Joyce Ndalichako pamoja na wanawake wengi walioko katika wizara mbali mbali wanafanya vyema sana kusimamia haki za wanawake na maendeleo ya wa Tanzania kwa ujumla

Mwaka huu wanawake tumeona maboresho Makubwa katika vituo vya Afya, zahanati, na kupunguza matukio makubwa ya kina Mama kujifungulia njiani na kupata uduma za kitabibu kuanzia kata mpaka hospital za rufaa jambo ambalo limesaidia kupungua vifo vya Mama na mtoto"

Amefafanua kwamba licha ya serikali ya awamu ya tano kutoa kipaumbele kwa wanawake kushika nafasi za juu serikalini pia wanawake kwa sasa wanajitambua na kujituma hasa katika kujiendeleza kielimu na kutatua changamoto za kifamilia

Joyce Kiria licha ya kuwa mwanaharakati za haki za wanawake amekuwa mwanamke mwenye uthubutu wa kufatilia matatizo ya wanawake na kuyaibua katika jamii na kujizolea umaarufu mkubwa na kuaminika na baadhi ya wanawake wamekua wakiomba kuona siku moja anakua katika wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto

Ili aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi kwani amekua mfano mkubwa wa kuigwa katika kuwasaidia wanawake kujitambua na kupambana kupata haki zao pale ambapo wanadhulumiwa na hata kushindwa kupata nafasi za uwajibikaji mpaka watoe rushwa ya ngono kwa waajiri wao

Wanawake wanajitambua wanawake ni jeshi kubwa tumeaminika na tusonge mbele katika kujenga uchumi wa nchi yetu

 
Naona ndugu zangu wengi hapa wameacha ujumbe wa msingi kuliko wote na kuanza kumshambulia Joyce Kiria. Ujumbe wa msingi kuliko wote hapa nadhani ni mwanamke kujitokeza kugombea nafasi za kisiasa kwenye ngazi mbalimbali za uongozi ndani au nje ya CCM. Kitu ambacho mtu yoyote yule muungwana, ambaye anapenda mabadiliko na maendeleo ni lazima akiunge mkono kwa nguvu zote.
 
Mimi ni mwanamke lakini siwezi kumkubali huyu Ngeetwa
Jifunze kutengenisha mtu na ujumbe, nadhani hili kama watanzania tukiliweza tutafika mbali sana. Unaweza kumchukia Joyce Kiria kwa tabia yake yoyote ile, lakini nadhani kama mwanamke ungekuwa ni mtu wa kwanza kuangalia kwa upana huu ujumbe aliouleta hapa na siyo kuanza kumkashifu Joyce.

Tunapambana na mfumo dume ambao umewaweka wanawake kwenye nafasi mbaya kijamii na kiuchumi. Hawa wanawake ambao Joyce anawaasa waje jugombea nafasi za kisiasa ndiyo wale ambao wanalea maraisi, mawaziri, madakatari na wanasayansi wa baadae: Hawa wanawake wakiingizwa kwenye mfumo mzima wa uzalishaji taifa hili lina uwezekano mkubwa sana wa kuwa lenye mafanikio na maendeleo huko mbeleni.

Ni ushauri tu mkuu, unaweza ukaubeba au ukauacha.......
 
Kwani nikichangia alichokisema ni lazima nichangie kila kauli yake? 😳
Mkuu BAK, unadhani unetenda haki kumhukumu binadamu mwenzako bila kupitia kauli zake zote alizozitoa ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…