Hii ni 'kero' mpya ya Muungano. Inaashiria kwamba siku za mbele jambo lolote ambalo linafanywa kimuungano litakuwa linaleta utata tu, suluhisho ni kila upande u mind their own business, every business, tunakataa ukweli tu Watanzania, tunakataa ukweli, watu wamechoka na Muungano. Mimi naamini kwamba hata baada ya Katiba mpya, muundo wowote ambao utakuja baada ya Katiba mpya haitakuwa mwisho wa 'kero' za Muungano. Kila siku itakuwa kuongelea kero za Muungano, kero, kero, kero...
Lakini Zanzibar ni sehemu ndogo sana ya Tanzania (Zanzibar haijazi hata robo ya Mtwara!) lakini ina distract national agenda ya nchi nzima, inakula national attention ya nchi, ya nini?
Wanadai Zanzibar haina wajumbe wa kutosha kwenye bodi ya NECTA, na Wamakonde nao tudai equal representation kwenye bodi ya Wakurugenzi wa NECTA?
Na Wasukuma nao wakidai? I mean, kuna Wasukumu milioni 5 unusu, Wazanzibari milioni moja, nani ana haki ya kudai equitable representation kwenye bodi ya Wakurugenzi wa NECTA, Wasukuma au Wazanzibar? Wazanzibari kwani wao nani?