Joyce Ndalichako, Katibu mkuu mtendaji NECTA maarufu zaidi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) halijawahi kupata tena Katibu mkuu mtendaji maarufu kuliko Prof. Joyce Ndalichako, huyu mama ilikuwa ikifikia wakati wa kutangaza matokeo ya NECTA ya darasa la saba, kidato cha nne au cha sita nchi inasimama.

 

Alikuwa ana misimamo yake thabiti isiyoyumba. Alikuwa Mtu wa Viwango na Ubora
 

Ndalichako hakuhusika na kusimamia baraza na kutangaza matokeo peke yake

Kabla ya kushika ile nafasi alihusika zaidi kulijenga upya baraza mitihani. Kuondoa mifumo yote ya ubadhirifu iliyochangia mambo mabaya kama wizi wa mitihani, na utengenezwaji vyeti feki na mambo mengine kama hayo

Ndalichako alifanya kazi kubwa kwa wakati wake
 
Wakati huo mnasikia one ya Saba zipo tatu tu Tanzania nzima, Leo st Francis wanafunzi wote wana one za Saba,na wanafunzi wote wamepata A masomo yote tisa kasoro physics tu.
 
Hamna katibu wa baraza alio kua Mdini kama huyu bibi, alikua anafanya mambo mengine kufurahisha ma boss wake, ndo maana wakati ulio fika aliondolewa mapema tu.
 
Hamna katibu wa baraza alio kua Mdini kama huyu bibi, alikua anafanya mambo mengine kufurahisha ma boss wake, ndo maana wakati ulio fika aliondolewa mapema tu.
Alifanya udini gani?
 
Ila hakuwa msafi, alikuwa anapita kwenye maofisi fulani fulani kukomba payback kwenye mafungu ya ukarabati
 
Enzi za huyu mama ukitoka na 1 au hata ka 2 ka mwanzoni umepambana ila sio sahivi aisee 1 mseleleko
 
Alifuta soma la dini ya kiislamu na kubadili arama zao huku akacha Bible knowledge
Somo la dini ya Kiislamu wanafunzi wanafundishwa kuhusu dini, Bible knoweldge wanafunzi wanafundishwa kuhusu Biblia na sio theology ya dini ya Ukristo ndio maana unakuta wakatoliki, Walutheri, Wasabato n.k wote wanachanganyikana pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…