Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Polisi zingatieni haki za binadamu maana yaliyoandikwa hapa hayatekelezwi nanyi vijana wa CCP Moshi.
 
Raia ana haki ya kujua elimu ya anayemkamata

Sijajua uhusiano uliopo kati ya raia aliyekamatwa (Mtenda au mshukiwa kutenda kosa) na elimu ya aliyemkamata (polisi). Nijuze nipate kuelewa.
 

Shukrani kwa kutujuza haki zetu za msingi. Keep it up!
 
Kama siridhiki na namna nilivyotendwa na polisi naweza kulalamika kupitia channels zipi? Kufungua shauri kawaida unaanzia polisi, je shauri la kumshtaki polisi linaanzia wapi?
 
Kama siridhiki na namna nilivyotendwa na polisi naweza kulalamika kupitia channels zipi? Kufungua shauri kawaida unaanzia polisi, je shauri la kumshtaki polisi linaanzia wapi?

Nimejaribu kucheki site yao, lakini haionyeshi ni jinsi gani ya kulalamika dhidi ya polisi. Kwenye nchi nyingine huwa wanakuwa na tume huru ambayo kazi yake ni kuhakikisha kuwa malalamiko dhidi ya polisi yanashughulikiwa ipasavyo. Unless kama kuna utaratibu mwingine, unaanza kulalamika kwa kupitia inspecta wa kituo chako cha polisi au kwa police staff manager kama yupo then unapanda ngazi taratibu. Lakini kama malalamiko ni mazito, sidhani kama hii ni njia muafaka.

Pia sidhani kama polisi wanaweza kuwa fair na unbiased ku handle complaints from a member of the public. Labda wadau wenye ufahamu na hili watasadia kujua taratibu za kuilalamikia polisi.
 
Naweza nikajua haki yangu nikikamatwa na polisi lakini nikijaribu kujitetea mbele ya polisi watasema wanafahamu wajibu waho,na wanajua sheria za kazi yao hapa cha maana tanzania akuna usawa na haki kwa nchi yetu pia tumezoe sana ruhwa ukisema ukweli ukimzidi atakwambia nipe kdogo kitu ndio tuelewane.
 
Rushwa ipo tz.lakini pia wabongo wengi aidha tunapungufu au hatujiamini kila tuingiapo mahali kuhitaji huduma hutanguliza kitu kidogo.Naamini tukiwa wasafi rushwa itakoma.
 
nashukuru umeweza kunifahamisha coz juz tu baadhi ya sheria hizo kuna police amezivunja
 
hongereni wachangiaji wote kuzidi kuelimishana ndio madhumuni ya jamii forum wala sio mipasho na matusi na lugha chafu
 
Dilunga

KWANI HAPO JIZI LINAKUWA LIMEKUJA KUSEARCH? KUKWIBA? HAPA LINALO ONGELEWA NI KUKAGUA SIO KUIBA
 
Polisi wakisha kukamata unakuwa wewe tena huna haki. Wao ndio wenye haki kwako wewe haswa hizi Nchi za Afrika zote. Afrika hakuna Haki za kibinadamu Polisi hana haki ya kukupiga akisha kukamata lakini wapi Afrika yetu Polisi ndio wamegeuka wao ndio Mahakimu badala ya Mahakimu wenyewe.
 
Mdau naomba ujue kwamba kuna upekuzi wa dharula ambao huhitaji search order soma S.42 34 ya CPA (R.E 2002) at page, kuna wakati polisi wanalazimika kufanya upekuzi huo kufuatana na mazingira ya kosa hivyo ni muhim ukajua hilo.

PILI, umezungumzia kwamba hati ya upekuzi hutolewa na mahakama but for my understanding search order ipo polisi na kuna mazingira court may issue search that is in practice kwa tz. just imagine kuna tukio limetokea j.mosi and search is needed to be conducted na mahakam hazifanyi kaz utafanyaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…