Jua kazi inayokufaa kulingana na tarehe yako ya kuzaliwa

Jua kazi inayokufaa kulingana na tarehe yako ya kuzaliwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
JUA KAZI INAYOKUFAA KULINGANA NA TAREHE YAKO YA KUZALIWA

siku ulio zaliwa inaashiria ni kazi gani ukifanya utapata mafanikio kimaisha, Mfano:-

numbers-colorful-clip-art.jpg



Kama umezaliwa tarehe 1 ya mwezi wowote wewe watu wanakuangalia na kukuhitajia sana kwa hiyo kazi zinazokufaa ni za siasa, msemaji katika shughuli mbali mbali Au MC , muigizaji, mtendaji na uelewe kwamba wewe umezaliwa kuwa kiongozi.

Kama umezaliwa tarehe 2 ya mwezi wowote wewe mahusiano yako na watu wengine yako kihisia zaidi kuliko kiakili na unaweza kuwa mwalimu wa elimu ya nafsi au mwanasaikologia, mtoa ushauri karani muuzaji.

Kama umezaliwa tarehe 3 ya mwezi wowote wewe ni mstahamilivu kwa watu wengine na unapenda kuonekana kwa hiyo unaweza kuwa mwalimu au mtu wa dini Sheikh au Padri au muimbaji au mhadhiri.

Kama umezaliwa tarehe 4 ya mwezi wowote wewe ni mtu mwenye bidii na juhudi na una hisia za ubunifu unaweza ukawa mjenzi mzuri au mkulima mzuri wa Bustani.

Kama umezaliwa tarehe 5 ya mwezi wowote wewe ni mtu mdadisi unaweza kuwa mwanasayansi, mwalimu au mtaalamu wa komputa, au kazi ambazo zinachanganya teknologia na kusafiri kama vile rubani wa ndege.


Kama umezaliwa tarehe 6 ya mwezi wowote wewe ni mtu wa furaha na unajua unachokisema kwa hiyo unaweza kuwa mshauri mzuri mtoa nasaha mzuri au muuguzi mzuri.

Kama umezaliwa tarehe 7 ya mwezi wowote wewe ni mtu mwenye maadili mema na hali ya juu muangalifu unaweza kuwa muandishi mzuri wa vitabu, Mwanasayansi mzuri na Mkemia mzuri.

Kama umezaliwa tarehe 8 ya mwezi wowote wewe ni mzuri katika Pesa unaweza kuwa mfanayabiashara mzuri, unaweza kuwa mfanyakazi mzuri wa Benki au ukiwa na uwezo unaweza ukaanzisha Benki yako au unaweza kuwa Mjenzi mzuri.

Kama umezaliwa tarehe 9 ya mwezi wowote wewe unapenda uhuru wa nafsi yako unaweza kuwa mtoa ushauri mzuri wa mambo ya kiroho na mponyaji.

Kama umezaliwa tarehe 10 ya mwezi wowote wewe ni mtu mkali mwenye jazba, mwanasiasa na kiongozi kwa kuzaliwa, unaweza kuwa mtendaji mzuri, mkurugenzi mzuri, daktari mzuri, msimamizi mzuri wa ubora wa bidhaa.

Kama umezaliwa tarehe 11 ya mwezi wowote wewe ni mtu mwenye hisia kwa wengine unaweza kuwa mwalimu mzuri au mshauri mzuri katika jambo lolote.

Kama umezaliwa tarehe 12 ya mwezi wowote wewe ni mtu uliyezaliwa mshairi au mtu wa kutengeneza mambo, shughuli zako ni za kumalizia miradi ambayo wengine hawajaikamilisha, ni mzuri katika kupatanisha na kuuza au udalali.

Kama umezaliwa tarehe 13 ya mwezi wowote wewe ni muuzaji mzurri mzuri ambaye una vitu vyote, kipaji cha kuuza na kuongoza, unafanikiwa katika nyanja za usanifu majengo, ubunifu wa miundombinu, siasa, na kuandika mipango ya miradi.

Kama umezaliwa tarehe 14 ya mwezi wowote wewe ni mtu ambaye una utaratibu mzuri wa kufanya mambo au kazi , unaweza kuwa mkandarasi mzuri, au meneja mzuri au katibu muhtasi, secretary.

Kama umezaliwa tarehe 15 ya mwezi wowote wewe ni mtu wa diplomasia na vile vile ni mtu ambaye una uwezo wa kujifunza na kujua lugha nyingi, unaweza kuwa Mfanyakazi mzuri wa taasisi za fedha, au balozi mzurri au mtafsiri mzuri

Namba 16 ni namba ya udhanifu (Idealistic) na Kama umezaliwa tarehe 16 ya mwezi wowote wewe unaweza kutoa huduma kwa jamii, au kufanya kazi za Bandarini kusafirisha na kupokea mizigo, kazi za uvuvi au kufanya kazi za ukarimu.

Kama umezaliwa tarehe 17 ya mwezi wowote wewe unapenda elimu unaweza kuwa professa au mshauri au daktari wa magonjwa ya akili au unaweza kuwa muandishi maarufu

Kama umezaliwa tarehe 18 ya mwezi wowote wewe ni mzuri katika kupanga mipango ya miradi na usimamizi. Utafanikiwa zaidi katika shughuli za mazingira, Ujenzi na ubunifu.


Kama umezaliwa tarehe 19 ya mwezi wowote wewe ni mbinafsi na mtu unayependa kuangalia mbele, teknologia ya habari inakufaa lakini unaweza kuwa mshauri wa mambo ya kiroho.

Kama umezaliwa tarehe 20 ya mwezi wowote wewe kwa asili ni mtu wa nyumbani na unaweza kuwa muuguzi, mtoa huduma au mtu wa kusafisha nyumba.

Kama umezaliwa tarehe 21 ya mwezi wowote wewe ni mtaalamu wa kushuku watu au mambo na mipango unaweza ukafanikiwa sana ukifanya kazi katika taasisi za fedha au viwanda vya uchapishaji.

Kama umezaliwa tarehe 22 ya mwezi wowote wewe ni mtu mwenye kuhisi na mwanasayansi kwa wakati mmoja, unaweza kuwa muuguzi wa ajabu au daktari au mtoa ushauri nasaha au msanifu majengo.

Kama umezaliwa tarehe 23 ya mwezi wowote wewe ni mtu mchambuzi unayeweza kusuluhisha au kushutumu, chochote unaweza kuwa mhasibu mzuri sana.

Kama umezaliwa tarehe 24 ya mwezi wowote wewe ni katika mwewpesi kuelewa kile ambacho watu wanataka unaweza kuwa wakili mzuri au mtaalamu wa elimu ya nafsi au saikologist.

Kama umezaliwa tarehe 25 ya mwezi wowote wewe ni asili yako ni mtu wa kiroho unaweza kuwa mshauri nasaha mzuri au mponyaji.

Kama umezaliwa tarehe 26 ya mwezi wowote wewe ni mfanya kazi hodari na una mbinu za kipekee za kupanga mambo na utafanikiwa kama ukiwa msimamizi katika nyanja yoyote ile..


Kama umezaliwa tarehe 27 ya mwezi wowote wewe ni mjanja na mwerevu, mwenye akili na si mtu wa kawaida unaweza kuwa mwana sayansi, au mambo yanayohusiana na mawasiliano au ukijafinyia kazi zakjo mwenyewe.

Kama umezaliwa tarehe 28 ya mwezi wowote wewe ni mtu mbunifu, mbinafsi na vile vile unapenda kusafiri, utafanikiwa sana ukifanya kazi za utalii au kufanya kazi zinazohusiana na wanyama

Kama umezaliwa tarehe 29 ya mwezi wowote wewe ni mtu ambaye unajali sana watu wengine na unaweza kufanikiwa sana katika nyanja ya tiba, vile vile unaweza kuwa mfanyisha mazoezi mzuri physical trainer au mtaalamu wa tiba maungo.

Kama umezaliwa tarehe 30 ya mwezi wowote wewe ni mtu waku bwabwaja, mwenye kipaji na una ubunifu wa asili. Utafanikiwa sana ukifanya kazi katika radio au television au katika uandishi na unaweza kungara kama ukiwa mwanariadha au mvumbuzi.

Kama umezaliwa tarehe 31 ya mwezi wowote wewe ni kiongozi wa kweli mwenye nguvu na unayejiamini una uhakika unaweza kuwa mchunguzi, mwanasayansi au mtafiti wa aina fulani. Vile vile unaweza kuwa Mjasiriamali mzuri na wengine watajifunza kutoka kwako.

Ukiwa na shida yoyote Au unataka Ushauri kuhus nyota,bahati pete ya mafanikio kushinda kesi kupata kazi, kuowa au kuolewa na matatizo yoyote yale usikose kunitafuta kwa kubonyeza hapa.
Mawasiliano
 
Back
Top Bottom