naona sio sahihi kwa sababu Afrika ya kusini tunakuita bondeni ingawa nako tunakatiza mawingu kufika. Nadhani hii ya majuu inatokana na ramani ya ulimwengu ilivyowekwa na kuonekana kama vile bara la Ulaya liko juu na bara la Afrika liko chini kwa hiyo kututia imani kwamba tuko chini ya Ulaya.Na kuhusu neno MAJUU, ilianzia kwa kufikiria kuwa mtu anakatiza mawingu yaliko juu, kama njia ya kwenda huko ulaya, na kwingineko.
Nimekusoma! Lakini: naona sio sahihi kwa sababu Afrika ya kusini tunakuita bondeni ingawa nako tunakatiza mawingu kufika. Nadhani hii ya majuu inatokana na ramani ya ulimwengu ilivyowekwa na kuonekana kama vile bara la Ulaya liko juu na bara la Afrika liko chini kwa hiyo kututia imani kwamba tuko chini ya Ulaya.
Ukitaka kutumia kiswahili fasaha, kuzama kwa jua ni Machweo na kinyume chake ni Mawio...! Hali hii ni muonekano wa chini ya upeo wa macho kama matokeo ya mzunguko wa dunia.Hivi ni sawa kusema jua limezama? Kama linazama huwa linazama wapi, manaake ukweli ni kwamba dunia ndio inayozunguka. Jua liko pale pale.
Unalo lizungumza ni sahihi, lakini kwa mtazamo wa kijiografia na haswa ukitazama ramani ya dunia, utaona kuwa nchi nyingi za ulaya zipo Kaskazini ya Afrika, hii ndio imepelekea kwa nchi za Ulaya tuzione kama zipo juu ya bara la Afrika (Kiramani).Mbaya zaidi wabongo tunatabia ya kuita Ulaya eti ni majuu, kama vile sisi tupo sehemu flani iliyoko chini. Kijeografia hii si kweli. Hakuna nji iliyeko juu bana. Huko juu kuna mawingu n.k!
Tafadhali changia tueleweshane.