Jua ndiyo kitu kikubwa zaidi kwenye mfumo wetu wa jua

Jua ndiyo kitu kikubwa zaidi kwenye mfumo wetu wa jua

dosho12

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
596
Reaction score
1,475
Wakati mabillioni ya nyota zilizo sambaa angani kwenye galaxy ya mlky way linapatikana JUA ambalo ndio muhimili wa mfumo wetu wa jua (Solar system). jua letu limetengenezwa takribani miaka billioni 4.5 iliyopita ilietengenezwa baada ya mkusanyiko wa gesi na moshi wenye vumbi vumbi inayojulikana kama Solar Nebula kusinyaa au kujivuta kisha kutengeneza kitu chenye umbo kama mpira lenye moto na gesi na kuwa Jua

Joto linalopatikana kwenye jua ukujumuisha na mvutano (Gravity) na mvutano wa sumaku (magnetic field) unasababisha jua kuwa na umuhimu mkubwa sana kwenye mfumo wetu wa jua

Jua linaweza kugawanywa kwenye safu sita {6} ambazo ni:

1. Corona
2. Chromosphere
3. Photosphere
4. Convective zone
5. Radiation zone
6. Core

Kwa upande wa Atom jua lina asilimia 91% hydrogen ambayo ndio kama mafuta yake kisha asilimia 8.9% helium na 0.1 heavier element kama carbon na nitrogen. Kutokana na joto kubwa lililopo kwenye jua hizi gas zipo kwenye mfumo wa uji uji wa moto unaoitwa [MAGMA]

Kwenye kiini cha jua (core) joto linafika mpaka nyzi joto { 27,000,000 F} sawa na {15,000,000 C} ukujumisha na gravity ya jua inaziunganisha molecule za hydrogen na kuwa helium mfumo unaoitwa {Thermal nuclear fusion} kisha hutoa nishati ( energy) ikiwa kwenye mfumo wa

1. Miozi (Radiation)
2. Umeme (Electricity)
3. Upepo wenye joto (Solar Wind)
4. Joto na mwanga na mwanga vinavyosaidia kuleta uhai duniani

Jua ndio kitu kikubwa zaidi kwenye mfumo wetu wa jua [ solar sytem ], ikiwa na upana mara mia ya dunia pia linaweza kujaza sayari zote nane zilizopo mara mia sita{600} na likichukua asilimia 99.8% ya uzito uliopo kwenye solar system huku asilimia 0.2% ikiwa ni vitu vyote vilivobaki.

Kutokana na uzito huo jua linatengeza mvutano mkubwa unaofanya sayari nane kuu, sayari ndogo ndogo kadhaa, miezi mia na sabini {170} ikiwepo mwezi wetu na vimondo vingi visivyo na idadi kuwa kwenye mzunguko wake ambapo Bila jua hivyo vyote vingesambaa na kuzagaa angani.

Kitu kingine cha muhimu kwenye jua ni mvutano wa sumaku {magnetic field} unaoitwa heliosphere unaolinda sayari kutokana na miozi hatari iliyopo angani.

Ingawa jua ni kubwa na lina nguvu ila halita ishi milele, takribani miaka bilioni 6.5 ijayo litaishiwa hydrogen ambayo ndio mafuta yake, litatanuka na kuchukua Mercury,Venus pia dunia kisha kusinya kuwa nyota ndogo zinazoitwa (white dwarf).

Kabla ya hapo jua litabaki kuwa muhimili wetu mkubwa kwenye gravity yake inayoshikilia mfumo wa jua, magnetic field inayotulinda na miozi ya anga pia nishati ya mwanga na joto yenye msaada kwenye maisha yetu.
 
Hahahaaaa...wanatumia mahesabu na principles za fizikia kupima kutoka kwa umbali wa sayari mbali mbali na nyuzi joto za sayari husika, muda wa mwanga/joto kusafiri, nguvu ya mvutano iliyopo nk.
Kuna kifaa kilitumwa kwa mbali kidogo na jua na ukuchukua vipimo vya kiasi gani miozi inayotoka na mwanga
nina swali zito niwaulize..?
 
kuna uwiano upi kati ya space na vitu vizito kupelekea kupatikana kwa gravity ama space kuwa curved....????
space ipo kama shuka hivyo kitu kizito kinafanya lile space kuingia na kusababisha vinavyozunguka karibu kuja kwake
 
Wakati mabillioni ya nyota zilizo sambaa angani kwenye galaxy ya mlky way linapatikana JUA ambalo ndio muhimili wa mfumo wetu wa jua ( Solar system ). jua letu limetengenezwa takribani miaka billioni 4.5 iliyopita ilietengenezwa baada ya mkusanyiko wa gesi na moshi wenye vumbi vumbi inayojulikana kama Solar Nebula kusinyaa au kujivuta kisha kutengeneza kitu chenye umbo kama mpira lenye moto na gesi na kuwa Jua

Joto linalopatikana kwenye jua ukujumuisha na mvutano (Gravity) na mvutano wa sumaku (magnetic field) unasababisha jua kuwa na umuhimu mkubwa sana kwenye mfumo wetu wa jua

Jua linaweza kugawanywa kwenye safu sita {6} ambazo ni
1.Corona
2.Chromosphere
3.Photosphere
4.Convective zone
5.Radiation zone
6.Core

Kwa upande wa Atom jua lina asilimia 91% hydrogen ambayo ndio kama mafuta yake kisha asilimia 8.9% helium na 0.1 heavier element kama carbon na nitrogen. Kutokana na joto kubwa lililopo kwenye jua hizi gas zipo kwenye mfumo wa uji uji wa moto unaoitwa [MAGMA]

Kwenye kiini cha jua (core) joto linafika mpaka nyzi joto { 27,000,000 F} sawa na {15,000,000 C} ukujumisha na gravity ya jua inaziunganisha molecule za hydrogen na kuwa helium mfumo unaoitwa {Thermal nuclear fusion} kisha hutoa nishati ( energy) ikiwa kwenye mfumo wa
1.Miozi (Radiation)
2.Umeme (Electricity)
3. Upepo wenye joto ( Solar Wind)
4. Joto na mwanga na mwanga vinavyosaidia kuleta uhai duniani

Jua ndio kitu kikubwa zaidi kwenye mfumo wetu wa jua [ solar sytem ], ikiwa na upana mara mia ya dunia pia linaweza kujaza sayari zote nane zilizopo mara mia sita{600} na likichukua asilimia 99.8% ya uzito uliopo kwenye solar system huku asilimia 0.2% ikiwa ni vitu vyote vilivobaki

Kutokana na uzito huo jua linatengeza mvutano mkubwa unaofanya sayari nane kuu, sayari ndogo ndogo kadhaa, miezi mia na sabini {170} ikiwepo mwezi wetu na vimondo vingi visivyo na idadi kuwa kwenye mzunguko wake ambapo Bila jua hivyo vyote vingesambaa na kuzagaa angani

Kitu kingine cha muhimu kwenye jua ni mvutano wa sumaku {magnetic field} unaoitwa heliosphere unaolinda sayari kutokana na miozi hatari iliyopo angani

Ingawa jua ni kubwa na lina nguvu ila halita ishi milele, takribani miaka bilioni 6.5 ijayo litaishiwa hydrogen ambayo ndio mafuta yake, litatanuka na kuchukua Mercury,Venus pia dunia kisha kusinya kuwa nyota ndogo zinazoitwa (white dwarf).

Kabla ya hapo jua litabaki kuwa muhimili wetu mkubwa kwenye gravity yake inayoshikilia mfumo wa jua, magnetic field inayotulinda na miozi ya anga pia nishati ya mwanga na joto yenye msaada kwenye maisha yetu
Wale wenye mawazo ya: 'hakuna mwisho wa dunia' waje hapa wajifunze kitu.
 
space ipo kama shuka hivyo kitu kizito kinafanya lile space kuingia na kusababisha vinavyozunguka karibu kuja kwake
najua so nachotaka kujua ni uwiano.. nini kinafanya space iwe hivyo
 
Acheni uongo nani alijua kwamba jua limeumbwa miaka bilion kadhaa iliyopita
Walipima muda wa miamba na athari ya vimondo vya kitambu ili kujua muda ya dunia kisha wakaja na conclusion kwamba dunia haiwezi survive bila jua hivyo jua na dunia vitakuwa vimetengenezwa muda mmoja
 
Naomba kujua kidogo kisabashi cha mawambi ya electromagnetic nini, kama kuna mawimbi yenye nguvu zaidi ya hayo?
 
Naomba kujua kidogo kisabashi cha mawambi ya electromagnetic nini, kama kuna mawimbi yenye nguvu zaidi ya hayo?
Sijui hasa yanatokana na nini ila najua ni charge za umeme zinapokutana na magnetic field ndio hutoa magnetic waves kama mawimbo ya radio, pia kwenye nguvu nahisi hakuna sababu hata miozi pia ni zao la electromagnetic waves
 
Back
Top Bottom