Jude Bellingham ni ishu ya muda tu kuuzwa bei kubwa

United ya Ferguson

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2021
Posts
3,132
Reaction score
6,353
Wachezaji wa Uingireza hawajawahi kuwa wa bei nafuu toka kizazi cha zamani hadi kizazi kipya, kutokea kwenye mishahara wanayolipwa hadi kwenye bei ya kuwauza sokoni. Kwanza Waingireza wenyewe wanajua kuwafanyia Uhamasishaji wachezaji wao ili wakiwa sokoni wauzike bei kubwa.

Ukishaona mchezaji wa Uingiireza ana jina elewa kabisa ukienda kumuhitaji unaenda kupasuka, haijalishi ancheza vizuri sana au kawaida. Kwa mfano rejea kwa John Stone kutoka Everton kwenda City, rejea kwa Jack Glearilish kutoka Villa kwenda City, rejea kwa Kyle Walker kutoka Spurs kwenda City, rejea kwa Rio Ferdinand kutoka Leeds kwenda Man United, mifano ipo mingi sana.

Mfano muangalie Leo Rashaford, watu wanamzihaka na wanamsema, ila linapokuja swala la kuuzwa bei yake unaweza kukimbia. Kuna kipindi Barcelona walipeleka ofa ya kumtaka Rashford, bei waliyotajiwa waliishia kujikuna vichwa tu!

Harry Maguire pamoja na shida zake zote alizonazo, timu yoyote Ile ikipeleka pua pale kumuhitaji bei itakayotajiwa huwezi kuamini kabisa kama ndio huyu Harry Maguire anayetukwana kila siku. Nenda kamguse Declan Rice wa Westaham, pesa utakayotajiwa huwez kuamini kabisa!

Dortmund baada ya kumuuza Sancho, Mr robot naona wameanza kutengeneza mazingira ya kuja kuvana pesa nyingne ya kutosha kutoka kwa kijana wa Uingireza Jude Bellingham.

Washajua kabisa hii ni pesa tena pesa ndefu kweli kweli, wao siyo wajinga kuanza kumkabidhi kitambaa cha unahodha. Washajua timu za Uingiireza zishaanza kutokwa na udenda kwa kijana wao, ni ishu ya muda tu Dormound anavuta mkwanja mrefu kotaka kwa huyu kijana wa Uingireza.
 
Hapo pana dalili ya kutapeliwa mtu kama walivyotapeliwa Man Utd kwa Sancho, average player kuuziwa mtu kwa bei mbaya.
 
Yote tisa kumi, Dortmund wanajua biashara ya mpira. Wanafaa kupewa tuzo kwa biashara hii. Wao makombe sidhani kama ni kipaumbele.
Dortmund na Ajax wapewe Mechi ya hisani kisha wakabidhiwe tuzo.
 
Huo upuuzi arteta hataki
watauziwa wajinga wa manchester na wale wa the blauzi
 
Huwa sielewi mtu analamika team za Uingereza kupendelea waingereza, kununua waingereza bei kubwa, kulipa waingereza mishahara mikubwa.
Afu mtu huyo huyo akiwa anaongelea Soka la bongo anasema tusipendelee wageni, tuembrace wazawa.......

Jamani ndio kwao hawana Pa kwenda, hata Maguire Uingereza ndio kwao. Na kiwango chake kucheza team ya Nyumbani ni sawa tu.
 
John stone kutoka everton alinunualiwa £47 million ....

Kyle walker kutoka spurs £52million ....
Mbona hizo ni bei za kawaida sana kwenye football....

Labda grealish tu .,.,
 
Ataenda kwa washikaji zake city
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…