Judgement kesi ya General Imran Kombe

Judgement kesi ya General Imran Kombe

MASEETO

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2013
Posts
261
Reaction score
86
Tafadhali Watanzania na wana JF, naomba mwenye Judgement (criminal) ya kesi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anisaidie, nina shida nayo ndani ya siku mbili hizi.

Huyu jamaa, inasemekana aliuwawa na Polisi walihukumiwa kifungo. Lakini nina haha kupata hukumu yao bila mafanikio.

Tafadhali, naomba kuwasilisha
 
wana jf, please, naomba msaada kwa mtu aliye na material facts ya kesi ya aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa Taifa lt,general imran kombe alyeuawa na police wawili
 
Dah mkuu maseto kesi ya KAMANDA KOMBE ninayo ile inayohusu assesment of damage ambayo ilifunguliwa na mke wa kamanda kombe [ROSSELEEN KOMBE AS THE ADMINISTRATIX OF ESTATE OF LIEUTENANT GENERAL HUSSEIN KOMBE Versus ATTORNEY GENERAL (1999)] , hii kesi ni ya madai ya fidia iliyofunguliwa na mke wa marehemu LIEUTENANT GENERAL KOMBE alikuwa anadai fidia ya sh.690,000,000/=, na hiyo kesi Nyingine japo siikumbuki vizuri ni ya REPUBLIC Versus JUMA NSWA &MATTABA(1995) kama sikosei mkuu unataka nikupe maelezo kidogo au? funguka mkuu.
 
Advocate J

Du! nilikuwa nataka criminal case judgement, nimesaka bila mafaniko, au kesi hii inausiri
 
The Case of ROSSELEEN KOMBE AS THE ADMINISTRATIX OF THE ESTATE OF LT. GEN. IMRAN KOMBE Versus ATTORNEY GENERAL(1999), hii ni kesi ya madai iliyofunguliwa na mke wa marehemu LT.GEN. IMRAN KOMBE kudai fidia juu ya kifo cha mumewe kutokana na miradi mingi kuzorota baada ya kifo cha LT.GEN. KOMBE kifo chake kilichosababishwa na maofisa wa polisi(kwa bahati mbaya) ambao waliagizwa kutoka dar hao wawili kwenda moshi kufuatilia hilo gari lililoibiwa(NISSAN PATROL) mali ya mfanyabiashara MR.LADWA kwa bahati mbaya gari alilokuwa anaendesha LT.GEN.IMRAN KOMBE lilikuwa linafanana sana na lile lililoibiwa huko DAR mali ya MR.LADWA sasa basi wakawa wanalifukuzia na kulipiga risasi kwenye tairi hivyo gari la LT.GEN. KOMBE likaserereka likaegama mahali LT.GEN. KOMBE alikuwa na mke wake(ROSSELEEN) wakajisalimisha lakini maofisa wa police wakafyatua risasi na kumpata LT.GEN.KOMBE defence walioitumia n Mistake of fact(section 11OF THE PENAL CODE ) lakini haikuwasaidia ! ROSSELEEN kombe alikuwa anadai 690 MILIONI! alipewa 300S
 
kwafaida yengu na wengine tupe maelezo zaidi pia kama alishinda kes huy mke wamarehemu?

Ninashukuru sana kwa maelezo,angalau napata mwanga sasa. katika kesi nataka kujua what could be the principle/ratio decidendi kwa askari anayeua kwa taarifa za kuambiwa, na hatimaye kugundua kuwa walio muua si yeye. Asante mkuu
 
Kifo cha Mkurugenzi mkuu wa Usalama Taifa Luteni Jenerali Kombe hakijawahi kuwa wazi kwa wananchi....

Na hata ilipotangazwa hiyo sababu kuwa mapolisi walimchanganya na Jambazi kwa mfanano wa magari yao hakuna wenye Akili kubwa walioridhika nayo.

Ni kama kutangazwa kuwa gari aina ya Benz aliyobebwa nayo Edward Sokoine ilipinduka. Benz kama ile na muundo ule kupinduka pasipo kupigwa bomu kwanza ni ajabu na hata Wajerumani waliiguarantee Tanzania kuwa haitapinduka kutokana na muundo wake na wakati ule wa 1980's viongozi wengi wakubwa wa ujerumani walikuwa wanatumia aina hiyo hiyo ya magari.

Kingine tena ni sababu ya kifo cha late Dr. Omary Ali Juma, kutoka chakechake Pemba..... kwamba alikufa na siri yake nzito ambayo ni bora alikufa nayo kuliko angeamka nayo siku ya tarehe 5, July 2011 wakati wa sabasaba.

Watanzania wana meengi ukiwasikiliza na kuona confusions katika baadhi ya vifo vya watu wao vipenzi hasa Sokoine mtu wa watu.

Mungu anajua zaidi kuliko sisi
 
Naomba kujua ukiachana na aliekua Mkurugenzi pale idarani aliekufa/alieuawa kwa tuhuma kama hizi za wizi ama zinazofanana na hizi ukiachana na Gen Imran Kombe kuna ambaye kihistoria aliuawa kwa kesi kama hii?? Wale waliokuepo idarani Enzi zile za baba wa taifa watupe historia Kidogo
 
Back
Top Bottom