Juhudi za Fistoni kalala Mayele zinatoa funzo kubwa kwa wachezaji wazawa nchini Tanzania

Juhudi za Fistoni kalala Mayele zinatoa funzo kubwa kwa wachezaji wazawa nchini Tanzania

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Juhudi na kujituma kwa jasho na damu ndiyo mafanikio makubwa kwa Fiston kalala Mayele "The Vibrater".

Mayele alikuja Yanga SC baada ya Yanga SC kumuuza Tuisla Kisinda kwenda RS Berkane.

Mayele huko alipotoka alikua siyo star sana kama hivi anavyoimbwa sana na kuogopwa sana na mashabiki wa Simba SC na kupelekea mpaka baadhi ya mashabiki kusema; "Ahsante Mungu kwa kumuondoa huyu kiumbe anayetunyima furaha katika ligi yetu."

Napomuongelea Fiston kalala Mayele ni kama jitu kubwa sana, liite "Unju bin uniq", linapokuwa kwenye pitch ni duzaster kwa mabeki na makipa wa NBC PL, lakini dude hili lina juhudi za kujituma, nidhamu na lenye uchu wa maendeleo na pesa pia kuweka kibindoni.

"Mimi nimekuja Tanzania kutafuta pesa na ndiyo maana napambana sana."

The Vibrater Fistoni kalala Mayele alisikika kwenye interview moja baada ya kuwahabarisha wanahabari namna gani ana uchu na matamanio ya kutengeneza mkwanja na ndiyo maana anafanya bora ili mabosi waendelee kumpa kandarasi nzuri na nono.

NALIA NGWENA kwa kutumia juhudi za Mayele na mafanikio aliyoyaonesha naona kabisa wachezaji wetu wazawa, kuna kitu cha kujifunza kupitia mwamba.

Wachezaji wetu wazawa wasibweteke kwa kufika Simba SC na Yanga SC na kuona kana kwamba wameshamaliza kila kitu na kuanza kucheza kifaza.

Kwani mafanikio ya mchezaji wa ndani ya ligi yetu wengi wao ni kucheza Simba SC na Yanga SC wanatakiwa kuondokana na hiyo akili watie juhudi.

Kwa heri The Vibrater Fistoni kalala Mayele, hakika umecha alama na elimu kubwa wachezaji wetu wazawa. Huna baya mwamba.

1689533470634.jpg
 
Mpira ni kama baiskeli, kana unaijuwa basi unaijuwa tu.

Hii ni nukuu nilimnukuu Amis Tobias Gaga au Gagarino.

Tatizo siyo juhudi tu, kwanza uujuwe mpira wenyewe siyo papatu papatu tu.
Nimeipenda hii comment,

Si kwamba wachezaji wengine hawajitumi bali wanalimitiwa na viwango vyao.
 
Lengo la timu za mpira ni biashara na moja wapo ni uuzaji wa wachezaji. Kwenye swala la Mayele wanaofaidika ni GSM
 
Juhudi na kujituma kwa jasho na damu ndiyo mafanikio makubwa kwa Fiston kalala Mayele "The Vibrater".

Mayele alikuja Yanga SC baada ya Yanga SC kumuuza Tuisla Kisinda kwenda RS Berkane.

Mayele huko alipotoka alikua siyo star sana kama hivi anavyoimbwa sana na kuogopwa sana na mashabiki wa Simba SC na kupelekea mpaka baadhi ya mashabiki kusema; "Ahsante Mungu kwa kumuondoa huyu kiumbe anayetunyima furaha katika ligi yetu."
Hata Madilu System anamkubali amemuimba kwenye muziki wake
Sikiliza muziki huu mpaka mwisho 👇
 
Lengo la timu za mpira ni biashara na moja wapo ni uuzaji wa wachezaji. Kwenye swala la Mayele wanaofaidika ni GSM
Ona uyu taahira wa ukoloni akili zake, kwaiyo pesa ya kumuuza mayele inaingia kwenye account ya gsm? Gsm wanamiliki timu gani labda? Au wanammiliki mchezaji gani labda? Na gsm ni nani pale yanga?
 
Back
Top Bottom